Mambo yanayofanya mwanaume akuweke moyoni




Kumekuwa na mahusiano mengi ambayo huanzishwa lakini hayafiki hatua za zandoa kama lilivyo lengo kuu la mahusiano. Hali hii inafanya wanawake wengi tuwe na wasiwasi katika mahusiano. Tumekua tukifikilia "Je, atanifanya niwewake wa maisha?" Lakini tunasahau kujiweka tayari kwaajili ya kuwa wanawake wa maisha.
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo humfanya mwanaume akuweke moyoni na akufikilie kuwa wewe ni wake wa maishani.

Tabasamu.


Kama unahitaji mwanaume avutiwe na wewe basi tambua vitu muhimu kuvifanya unapokuanae ni kutabasamu na kucheka. Usionyeshe uso usio na urafiki. Kuwa kama mtu anayependeza, mwenye urafiki, na mchangamfu.

Kuwa mcheshi.



Wanaume kwa ujumla wanapenda wasichana wenye ucheshi ambao wanaweza kuwafanya wajisikie vizuri. Mwambie hadithi za kufurahisha, na usiogope kucheka. Kumbuka usizidi kupita kiasi hadi uonekane kama mchekeshaji. Ni vizuri kuwa na mwenzi ambaye anafurahisha, lakini ni watu wachache sana wanamawazo ya kuishi na mchekeshaji.


Toa kuliko kuchukua.



Ili kuongeza nafasi zako za kukupenda lazima utoe kuliko kuchukua. Mwanaume anaweza kutofautisha kwa urahisi kati ya msichana ambaye anataka kitu kutoka kwake na yule anayemjali.
Nadhani unajua kuna wasichana ambao wanafuata pesa (wauzaji). Jitofautishe na wauzaji na aone unavutiwa naye kwa upendo wake na sio pesa yake au kitu kingine chochote.


Mpenafasi ya kuwambali na wewe na kufanya kazi.



Kama muko kwenye mahusiano na mwanaume na anaonekana kuwa busy sana na kazi mpaka anafikia kuwa mbali na wewe,usimfikilie tofauti. Mruhusu mwanaume afanye kazi kidogo ilikufanya maendeleo Kisha vumilia pindi anapokua mbali na wewe ila usijisahau kumuonesha upendo zaidi na zaidi. Hili ni jambo ambalo linaweza kuongeza sana nafasi zako za kushinda upendo wake. Wanawake wegi wanakata tamaa na kumuacha mwanaume wanapoona yupo busy Sana na maisha huzani kuwa hawana nafasi tena lakini jua kuwa wakati huo ndio wakati mzuri wa wewe kuongeza upendo wake kwako.
Muoneshe kuwa bado yupo moyoni wako, muoneshe kuwa unajua anachokifanya, uulize maswali au kumshauri, muoneshe kuwa bado unamjali hii itamfanya akuweke katika fikila zake za kimaisha. Usijekosa maisha mazuri anayokupambania kwa kukata tamaa.


Usimmiliki sana kuliko kumuonesha upendo.





Wanawake wengi hufanya makosa ya kumiliki sana mwanaume na wakati hata hawamuoneshi upendo. Unaweza kujaribu kumlinda sana asiende kwa wanawake wengine ili abaki kuwa na wewe pekee katika maisha yake lakini je anao wafuata wanamvuta kama jinsi unavyo fanya wewe?. Ni wazi kuwa wanamvuta kwa upendo na vitu vingine vizuri... hivyo na wewe kuwa mbunifu na kwenye kumuonesha upendo ambao utamvutia zaidi kisha mruhusu aamue kuchagua kinachomfaa. Ikiwa wewe ndiye wa kwake, hakika atakupenda.

Kuwa na maadili mema.




Maadili mazuri ni lazima katika kumshawishi mwanaume akupende zaidi na aweke moyo wote kwako. Hakuna mtu anayetaka kujihusisha na mtu ambaye haeleweki,hasikii au hana nidhamu. Bila shaka kila mtu husita kumpa moyo mtu ambae hana maadili mazuri. Wanaume wanapenda wanawake ambao wana nidhamu. Hivyo basi muheshimu na pia uwevizuri nae ataona unafaa kuwa wake maishani.

Previous Post Next Post