Agano: 05 (Simulizi)






MTUNZI: CLEMENT CHARLES


……..General alionekana amechanganyikiwa kabisa asijue ni lipi la kufanya kwa muda ule huku sisi tukiwa tayari kusikiliza tamko lolote la mkuu kwani yeye ndie pale alikuwa na uzoefu kutushinda sote pale ‘’attention atiziii’’ ‘’kaeni tayari kuianza safari hii kwa miguu kwani kwa anga imeshindikana kifuatacho ni kufa na kupona’’ ‘’ndio mkuu’’, ‘’liutenant Mike kwa anga unanipataa’’ ‘’ndio nakupataa mkuu’’ ‘’rudini mpaka mpakani mwa Nigeria na niger tuwakuta hapo hiyo ni amri over’’ ‘’nimekukopi mkuu over’’. Safari ilianza kutoka eneo lile kuanza kuitafuta njia ya kuelekea mpakani mwa nchi ya Nigeria na niger (niger ni nchi iliyopakana na nchi ya Nigeria yaani ni kama vile Tanzania na Uganda) tulianza kutembea huku idadi ya mateka tuliowaokoa ikiwa ni watu kumi na mbili watatu wa Nigeria na waliobaki ni raia wa Tanzania mimi ndiye niliyepewa jukumu la kuwa mstari wa mbele kuviongoza vikosi vyote kutoka ndani ya msitu ule wa waasi nami sikulikwepa jukumu niliendelea kuvifyeka vichaka huku nikizidii kuitengeneza njia ya kuelekea mashariki.
Ghafla cheni niliyopewa na baba wakati naaga nyumbani kwa ajili ya kuja Nigeria iliyofanyiwa matambiko ya kila aina ilianza kutoa kitu kama joto na kuanza kunichoma kifuani kwangu haraka haraka nilijua tu hii ni hatari nilitoa amri kwa wanajeshi wote ‘’simama lala chini’’ wote walifanya hivyo na kutulia kisha nikatoa ishara ya kwenda huku tunaburuza tumbo kama nyoka (ku craw) bila kupiga kelele ya aina yeyote , kabla hata hazijapita dakika mbili tulihisi kishindo kikipita kando yetu kujaribu kuangaza tuliona mtu mrefu ambae hata kichwa chake hakikuweza kuonekana tulijikaza kijeshi huku nikiishikilia cheni yangu na kusema kimoyomoyo ‘’mizimu ya upande wa baba yangu na mama yangu naomba msimame nami msiniache niokoeni katika hiliii ewe mola wetu tuepushe katika hili amiin’’ wakati nikiyasema hayo wanajeshi wengine walikuwa wakiomba kwa sala zao mpaka yule kiumbe mrefu alipopita maeneo yale nami baada ya kuona kaishilia kabisa na haonekani nilitoa ishara ya kuwasimamisha wanajeshi wote na kuanza safari upya ya kuendelea kuutafuta mpaka.
‘’Brigedia pele kutoka makao makuu ya jeshi la wananchi Tanzania misheni kuokoa mateka Nigeria General Daitus mnanipata over’’ ‘’tunakupata vyema makao makuu over’’ ‘’ni amri kutoka kwa mkuu wa majeshi hakikisheni hao watanzania wanafika salama nchini over’’ ‘’tumekukopi brigedia Pele toka makao makuu over’’, yalikuwa ni maongezi kati ya general na makao makuu ya jeshi ambapo general alipokea amri mpya ya kuwapeleka wale mateka Tanzania na sio kuwaacha ndani ya nchi ya Nigeria.
‘’Sergeant Gedi simama’’ nilitii amri kutoka kwa mkuu ili kusikiliza nini kinachotaka kusemwa ‘’itabidi tupumzike hapa ndani ya robo saa afu ndipo tuendelee na safari au mnasemaje vijana wangu ‘’ndio mkuu’’ tuliitikiaa wote, ‘’ila we sergeant Gedi itabidi upande mtini kutuangalizia usalama ili tusije kufanyiwa ambush hapa nawewe sergeant Danny itabidi ulinde huu upande tunaotokea Sergeant Gedi atatuangalizia kwa upande wa anga kama uko sawa wengine tupumzike hapa’’ ‘’sawa mkuu’’. Nilijibu vile kisha nikaangalia mti wa kupanda nikaona mti mrefu afu mweupe nikaamua nikaupande huohuo ili kuona vizuri mi kama mlengaji wa masafa marefu, niliukwea ule mti na ndipo nikatafuta tawi zuri la kujiweka sawa ndipo nikaiseti bunduki yangu tayari kuangalia wapi atakapotokea adui. Niliichukua darubini na kuanza kuangaza angaza maeneo ya ule msitu huku ukiwa umetaradadi sauti za ndege nzuri nzuri nilianza kuangaza huku na huku mara ghafla nilipata kizunguzungu kilichofanya nipoteze fahamu na kushindwa kushikilia lile tawi vizuri huku nikiwa sijielewi nilidondoka toka juu ya mti mpaka chini puuh!!!!

JE NINI KILIMFANYA SERGEANT GEDI APOTEZE FAHAMU AKIWA JUU YA MTI? ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU INAYOFUATA KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH..
Previous Post Next Post