App 5 bora za kuplay musiki (Android)
1. AIMP
Hii ni app bomba na ina sifa nyingi sana ambambazo ni pamoja na kukupanafasi ya kuchangua app hiyo iwe na rangi gani. App hii inapatikana play store bure kabisa.
2.BlackPlayer EX
App hii si ya bure. Ili kuiinstall kwenye simu yako itahitajika kulipia kiasi cha pesa. App hii inasifa nyingi sana na nzuri pia, ndiomana inakubidi uilipie ili uitumie.
3. JetAudio HD
JetAudio HD ni app bomba iliotulia na wengi hupenda kuitumia kutokana na sifa za kuvutia zilizopo kwenye app hiyo. App hii hupatikana bure katika play store lakini utahitajika kuilipia ili upate baadhi ya sifa zake nzuri.
4. Mediamonkey
Hii ni app nzuri katika kuplay na katika muonekano. App pia inapatikana bure katika paystore yaani bila gharama yoyote. Lakini kunabaadhi ya sifa utazikosa mpaka utakapo lipia kiasi cha pesa.
5. Medialet
App hii ni moja kati ya app nzuri katika kuplay muziki na pia uzuri wa app hii ni kwamba Haina Ads. Hivyo basi utumiapo app hii usitegeme kusumbuliwa na Ads hatakidogo.