Abunuasi: Mlinzi (Simulizi fupi)

 





Abunuasi alikua anashinda ya kuonana na Mfalme. Kufika mlangoni kwa sultani mlinzi akakataa kumruhusu aingie kumwona.
Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi akakubali na akaingia kwa sultani.
Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani? Abunuwasi akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe. Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu yake kwa hiyo hivyo hamsini vilivyobaki atandikwe mlinzi. Sulatani kusikia hivyo akaghadhabika sana na kuamuru mlinzi aletewe apigwe viboko hamsini tena vya uhakika. Mlinzi alijuta kuzaliwa, na hakurudia tena kuomba rushwa.
Previous Post Next Post