Kama unahitaji game zisizo na ukubwa basi hizi ni game usizotakiwa kukosa kuzicheza.
1. Death Invasion
Ni game ambalo linamuonekano mzuri wa 3D na pia ni moja kati ya magame ambayo hupendwa na watu. Mpaka sasa game hili limechezwa na watu wasiopungua milioni 10 na asilimia 96 wamelipenda game hili. Game hili huusu zombies, kwa upande mwingine naweza liweka game hili katika game bora za zombies. Inashauriwa game hili lisichezwe na watu walio na umri wa miaka 18.
Death of Invasion ni miongoni mwa magame ambayo hupatikana kirahisi. Game hili hupatikana playstore na Kama unataka kulipakua, unaweza rahisisha zaidi upatikanaji wake kwa kugusaINSTALL
2. Last Human On The Earth
Kama ni moja kati ya watu wanapenda zaidi game zenye mazingira yenye uhalisia basi game hili linaweza kuwa moja ya game zako pendwa. Game hili hinahusu mtu ambae anaishi pekeyake katika ulimwengu na anakumbana na vitu vya ajabu. Watu milioni moja tu ndio waliolicheza mpaka sasa na asilimia 74 wamelipenda. Katika ukubwa, game hili ni dogo sana yaani unaweza lipakua kwa 24Mb lakini ubora wake upo juu kiasi. Watu wenye umri chini ya miaka 16 hawashauriwi kucheza game hizi.
Pia game hili hupatikana playstore. Unaweza kutafuta kwa kuliandika jina lake au unaweza pakua kirahisi kwa kugusa hapa INSTALL
3. Zombie city
Zombie city ni game lililotulia na linaweza kuwa katika orodha ya magame mazuri ya zombies. Halitumii data katika kulicheza. Asilimia 80 ya watu milioni wamelipenda game hili. Inashauriwa mchezaji wa game hili asiwe na umri chini ya miaka 12.
Lina patikana playstore. Kama utaliitaji unaweza pakua kirahisi kwa kugusa hapa INSTALL