Umekua ukiitaji game zinazohusiana na zombie kwaajili ya simu yako ya Android?
Kwenye post hii nakuorodheshea baadhi ya games zinazopatikana playstore zinazohusiana na zombies.
1. Dead Trigger 2
Ni moja kati ya magemu mazuri sana ambayo hupendwa na huchwezwa na watu wengi duniani. Game hili limechezwa na zaidi ya watu milioni 10. Watu wengi hulipenda game hili kutokana ubora katika muonekano pamoja na stori nzuri ya aina yake.
Unaweza kulipata kwa kutafuta katika app ya Playstore au gusa INSTALL
2. Unkilled
Ni game ambalo hupendwa na watu pia. Mara nyingi watu hulisifu kwa kutazama muonekano wake pamoja na stori yake iliotulia. Game hili ni zuri lakini pia linatisha kutokana na uhalisia flani walio uweka katika game.
Ukiitaji game hili unaweza kulipata katika app ya Playstore au Kama Ni mpenzi wa magame mod basi unaweza kutafuta Google pia unaweza gusa INSTALL