Kama ni mpenzi wa muda wa kuangalia mpira wa miguu, nadhani umeshawahi kosa kuangalia mechi ulioipania kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwa mbali na Tv.
Teknolojia inazidi kukua kila siku na kuturahisishia mambo. Sasa unaweza angalia mechi Kali za mpira wa miguu kupitia simu yako mubashara(Live) ukiwa popote.
Ikiwa unahitaji kuangalia mpira kwenye simu yako, utahitajika kuwa na app maalumu kwaajili ya kuangalizia mpira. App hizi zipo nyingi sana katika playstore(Android) lakini mimi nakushauri uchukue app nyepesi na isiokula sana Mbs iitwayo Live Football Tv.
App ya Live Football Tv ni app ya bure ya kuangalizia mpira ya nje live. Mpaka Sasa inatumiwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10) ulimwenguni na wanaisifu kwa kuonesha mipira mingi bila matatizo. Mbali na kukuonesha mechi live(mubashara), huwa inakupa matokeo na video za matukio muhimu ya mechi zilizomalizika kwaiyo Kama haukua na bando la kutosha kuangalia mpira mzima, unaweza angalia video ya goli lilivyofungwa tu. Pia inakupa nafasi ya kuangalia vipindi vingine vya kimichezo bure toka Ptv sports.
App hii inapatikana playstore kwa MB7. Baada ya kuipakua, hauitajiki kujisajili au kufanya Jambo lolote la kujiunga. Unaweza ipakua kirahisi kwa kugusa INSTALL
Je, ni Mbs ngapi zinahitajika kuangalia mpira mzima(Dk90) kwenye simu?
Hili ni swali ambolo wengi hujiuliza, wanapohitaji kuanza kuangalia mpira kupitia simu. Ukweni ni kwamba, kadri video inavyokua na muonekao mzuri ndivyo Mbs huwa zinalika nyingi. Itakua ni vizuri zaidi Kama hautakua na chini ya Mb900 ili kutokua na wasiwasi wa bando kuisha.