KIKUNDI CHA WATALII kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: "Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10". Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe "Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu". Mke wake akatabasamu na kusema "Ni mie ndio nilikusukuma". Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Anyway, "Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio".
UMEMUAGA mkeo unaenda kazini, ukapita kwa mchepuko wako, wakati unajimwaya-mwaya na mchepuko, mume wa mchepuko akagonga mlango, ikabidi ufichwe uvunguni mwa kitanda.
Wakati bado upo uvunguni ka mchepuko kakamuaga mume wake kwamba, kanaenda saloon, mume wa ka-mchepuko naye akaona ndo muda wa kuita mchepuko wake, akauita ukaja, wakajimwayamwaya kwa sana muda huo wee bado upo uvunguni. Mara mchepuko wako akarudi kutoka saloon, akagonga mlango, ikabidi mume wa mchepuko wako aufiche uvunguni mchepuko wake.
Kucheki hivi kumbe mchepuko wenyewe ndo mke wako uliyemuaga unaenda kazini, kwa hiyo wewe na mke wako wote mkawa mmefichwa uvunguni...Ukisikia vita ya tatu ya dunia, ndo hii sasa.