Magroup ya WhatsApp yanaweza kuwa sehemu nzuri ya jumuika na kubadilishana mawazo lakini vile vile magroup ya WhatsApp yanaweza kutumika Kama chanzo cha kuingiza pesa vile vile.
Kuna njia nyingi sana unaweza zitumia ili uingize pesa kwa magroup ya WhatsApp. Njia hizo zinaweza kuwa ni kulitumia group la group la WhatsApp kama soko la bidhaa zako na kutumia group la WhatsApp kama chanzo cha clicks au views lakini njia hii unahitaji ujuzi kidogo. Njia rahisi ambayo kila mtu anawezakuifanya ni kutumia group la WhatsApp kama soko yaani kuweka group la WhatsApp liwechanzo cha wateja wa bidhaa zako. Fuata hatua hizi ili kutengeza pesa kwa njia hii.
1. Tengeneza group la WhatsApp la burudani.
Watu wengi hukosea hapa. Watu wengi wanaohitaji kufungua magroup kwaaji ya kutangaza biashara zao hufungua magroup yanayohusu biashara zao tu na magroup mengi ya muundo huu hayadumu kwa muda mrefu kutokana na watu kutoshawishika kufungua mara kwa mara group hilo. Fungua group la burudani yaani group la Simulizi, Vichekesho au michezo. Ikiwezekana katika jina la group liwe na jina la biashara yako ( Mfano: Vichekesho & Nguo mpya)
2. Sambaza Link ya mualiko.
Chukua link ya kujiunga na uisambaze katika magroup mengine ulionayo au katika mitandao mingine ya kijamii ili kuwapata members. Kama biashara yako inahusisha watu wa eneo flani basi hakikisha unasambaza link katika watu wa eneo hilo. Mfano Kama biashara yako inahusu watu wa Dar, nenda katika magroup ya Facebook ya yanayokusanya watu wa Dar kisha post link yako ikimbatana na maneno mazuri ya kumshawishi mtu aingie kwenye group lako la burudani alafu usisahau kusisitiza kuwa ni kwa watu wa Dar tu!.
3. Anza kupost burudani ili kuwalidhisha member wako.
Ukimaliza kusambaza link tu, utaanza kupokea members. Anza kutuma vitu kulingana na group ulilofungua. Yaani kama ulifungua group la Vichekesho basi anza kutuma Vichekesho na kama ulifungua group linalohusisha michezo basi anza kupost vitu vya kimichezo vitakavyowavutia member wako.
4. Anza kupost matangazo yako.
Baada ya kuwapa members wako vitu vinavyowaburudisha, Anza kupost matangazo ya biashara yako huku ukiendelea kuwapa burudani zinazohusiana na group ila hakikisha matangazo hayazidi maana yanaweza sababisha mtu kulichukia group.
Kwa wataalam wa clicks na views, hii pia inawezakua njia nzuri unachotakiwa wewe ni kufuata hatua hizo lakini hapo mwishoni badala ya kuweka matangazo unaweka links.