Watu wengi tunaingia kwenye mahusiano kwa sababu kuna kitu au vitu vilituvutia kutoka kwa wapenzi wetu lakini hiyo haitoshi inabidi muingie kwenue mahusiano na mtafute njia za kuweza kupendana na kuheshimiana kwa wakati mmoja ili muweze kudumu.
Katika kuhakikisha hilo leo nakuletea mambo 5 muhimu ya kufanya ili mapenzi yako na mpenzi wako yadumu:
1. Mawasiliano kwa ujumla
Kwenye mapenzi maongezi ya mara kwa mara na ya dhati na ni kitu muhimu sana. Ni muhimu kwa wapenzi kukaa chini na kuongea itasaidia kuwaleta pamoja na nyie kufahamiana vizuri na kila mmoja atajua nini kinaendelea kwenye maisha ya mwenzake.
2. Utayari wa kuvumiliana
Ili mapenzi yenu yadumu ni lazima wewe na mpenzi wako mjidhatiti katika kivumiliana hasa mkigombana au mkipitia magumu yoyoye kimaisha huuikimaanisha ili uhusiano wenu udumu ni lazina kila mmoja amvumilie mwenzake sio mmegombana kidogo tu unataka muachane au mmekosa pesa basi unataka ukamtafute mwingine.
3. Kukiri kosa na kuomba radhi
Ili mapenzi yenu yadumu lazima mjue kuna kukosea na ni muhimu pale unapokosea umuombe mpenzi wako msamaha hii itawasidia kiheshimiana zaidi. Wote tunakosea hakuna binadamu mkamilifu hivo ni muhimu kujifunza kutoka kwenye makosa yetu.
4. Kuheshimiana
Hakuna kitu muhimu kwenye mapenzi kama heshima ni minimum kila mmoja amheshimu mwenzie hii itasaidia kuweka mipaka fulani katika mahusiano na hii itoke pande zote mbili mwanamke amheshimu mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.
5. Jengeni Urafiki
ili mapenzi yenu yadumu ni lazima muwe na ukaribu na urafiki ili muweze kuwa karibu na ili mpenzi wako aweze kukwambia kitu chochote ni lazima mjenge ukaribu ilmuambiane kila kitu lakini hapa pia muwe makini Latina kiwe na mipaka ili msije shindwa kufanya mambo yenu mambo yenu.