MTUNZI: CLEMENT CHARLES
INAENDELEA;
………..Tulijiachia hewani huku kila mmoja akilicontrol parachute lake vyema kuelekea upande alioelekezwa na general mimi nikiwa kama kiongozi wa Team Rhino tulitua katikati ya msitu uliotulia tukifuatiwa na Team Wolf ambayo ilikuwa chini ya sergeant Danny baada ya kutua wanajeshi wote tuliokuwa nao kila team ilijumuisha wanajeshi sita sita. Kama alivosema General wetu Team Wolf walianza kuelekea upande wa mashariki namimi nikaanza kukiongoza kikosi changu kuelekea magharibi nia na lengo kuu ni kumuweka adui yetu kati huku tukitembea kwa umakini mkubwa kama wanajeshi pekee tuliochaguliwa kutoka Tanzania kwenda kuwaokoa mateka waliokamatwa na Waasi nchini Nigeria .
‘’Team Wolf mnanipata over’’ ‘’tunakupata vizuri kabisa sergeant Gedi over’’ ‘’tushaaifikia kambi ya waasi tunasubiri order over’’ ‘’nasisi tushaiona tunasubiri order kutoka kwa general over’’ ni mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Team hizi mbili katika operation yao ya kijeshi nchini Nigeria wakisubiri order kutoka kwa General wao ambae alikuwa kimya mpaka dakika hiyo. ‘’Team Wolf tumeangalia kwa darubini tumefanikiwa kumuona General akiwa ametekwa na waasi sa kuweni makini kwa upande wenu pia kifuatacho ni kuvaamia kambi na kuwatoa mateka pamoja na Team Alpha yote over’’ ‘’nimekupata team Rhino over’’ . Baada ya kutoa taarifa ile nilianza kukipanga kikosi changu tayari kwa kuivamia kambi ya waasi illiyokuwa inaonekana imejizatiti sana kutokana na kutumia silaha nzito za kivita kujilinda, tangulieni mi nitakuwa nyuma yenu kuwasafishia njia hakikisha unapiga pigo moja na kummaliza adui sa chagua adui akumalize au wewe umumalize hiyo ni order over.
Tulitawanyika kisha mimi nikapanda juu ya mti ili kuwapunguza maadui kwa kutumia bunduki yangu ya masafa marefu, nilichukua tena darubini kisha nikawaona waasi wawili waliokuwa lindo wakiilinda ile kambi kwa upande wa maghaibi wakicheza karata huku wakivuta bangi, niliichukua bunduki yangu kisha nikaiweka usawa wa nilipokuwa kwenye ule mti kisha nikawaweka target vizuri alafu nikaivuta triga tayari nikaachia risasi ambayo haikutoa mlio kwani ilikuwa na silencer na kumpata mmoja wa waasi wale bila kupoteza muda nilimwelekezea upande aliopo yule mwingine na kufyatua tena risasi iliyompata moja kwa moja kichwani nayeye pia alianguka chini na kutulia tuli kama maji mtungini.
‘’Team Rhino nishawasafishia njia haya endeleeeni kusonga mbele over’’ ‘’tumekupata mkuu over’’. Wakati vijana wa Team Rhino wakisonga mbele waliona mti uliokuwa ukiyumbishwa na upepo wenyewe tu katika maziringira yale jambo ambalo lilifanya mmoja wao kutoa ishara ya kuwasimamisha wenzake ili kutoa maelekezo , ‘’hii ni team Rhino over’’ nikawajibu ‘’nawapata over’’ ‘’mkuu naomba uangalie sehemu tuliyopo kuna tatzo mti unapelekwa pelekwa na upepo over’’ ‘’sawa nachunguza over’’ ilibidi niweke bunduki chiini na kuanza kuangaza angaza maeneo waliyopo wanajeshi wa kikosi changu cha team RHINO kwakweli nilichokiona ilibidi niache kuangalia kwa muda lile jambo kwani nilichokiona ni tofauti na nilichoambiwa.
JE SERGEANT GEDI ALIONA NINI USIKOSE SEHEMU IFUATAYO.