Baba mmoja, baada ya kuwashwa na hela aliamua kununua roboti ambalo kazi yake ni kumtambua mtu anayesema uongo kisha kumzaba kofi hapo hapo. Alilichukua na kwenda nalo nyumbani kwake.
Siku moja akiwa anamfundisha mtoto wake nyumbani mambo yalikua hivi;
baba: 2 x 2 jibu lake nini?
mtoto; 10
roboti hapo hapo likamzaba kibao mtoto.
baba akajisahau na kuanza mfokea mtoto wake kwa hasira.
baba: unajua kipindi nasoma mimi sikuwa mjinga kama wewe! nilikuwa wa kwanza kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba
sio wewe mpumbavu hujui hata hesabu rahisi kama hiyo.
ghafla akapokea kibao kutoka kwa roboti mtoto akaanza kumcheka baba yake jinsi kibao kilivyomungia
Akatokea mama yake toka jikoni ili kuja mkanya mwanae kwa aliokua anayasikia
mama: ivi wewe mtoto umekuaje siku hizi? Yaani una mcheka baba yako mzazi!
kikasikikika kibao baba kuangalia ni mke wake ndio kapigwa na roboti
NILIAMUA KUONDOKA SIKUTAKA USHAIDI WA KESI YA AINA YEYOTE
UKITAKA UTAJILI TUMIA HII AKILI...
Msukuma aliamua kufungua bustani ya wanyama akafanya kiingilio 10,000/= hakuna aliyeingia akashusha 5,000/= pia hakuna aliyeingia akashusha tena 2,000/= hakuna aliyeingia akashusha 1,000 pia hakuna aliyeingia akaamua kufanya bureeeee watu wakaingia na walikua wengi mno akafungulia Simba mmoja akafanya bei ya kutokea nje ni 20,000/=
WIZI WA CHUPI...
Mwenye Kampuni kubwa ya kuuza chupi ukitaka "kocho ' alianza kulalamika chupi zake zilikuwa zikipotea kila siku baada ya wafanyakazi kuondoka makwao. Siku ya pili, chupi za kiasi milioni sita zilitoweka. Mkuu wa Kampuni aliitisha kikao kuanzia kwa meneja, na washiriki wote wa Kampuni hiyo. Hakuna aliyejua wala kujulikana mwizi alikuwa nani. Kila jioni Mkuu wa Kampuni alikuwa akikagua kila mfanyikazi ikiwa atamkuta amevalia chupi zaidi ya moja. Lakini la, hasha! Nani apatikane? Lakini binti mmoja mpishi katika Kampuni alijitokeza, 'Mkuu, bwana mbona usiwakague wafanyikazi wanapoingia kazini kutoka nyumbani? "Siku iliyofuata, Mkuu alijaribu kuwakagua tena walipoingia kazini. Salalee! Kumbe, alikuwa akichezwa chini! Alipata wafanyikazi wake kwa waume walikuwa tupu bila chupi! Kumanisha zile chupi walizoiba walikuwa wakivaa jioni wakirudi makwao. Mkuu wa Kampuni hakuwa na la kusadiki ila kumshukuru Yule binti. Alimtuza Yule binti cheo akawa meneja wa Kampuni hiyo! Kutoka jikoni hadi afisini. madaraka yaloje? Kweli ukitaka kuendelea fanya mambo kitofauti usifanye mambo tofauti.