MTUNZI: CLEMENT CHARLES
INAENDELEA;
………Mpambano ulianza kwa yule mwanajeshi wa kiasi kuruka teke zito lililompata mwanajeshi wa kitanzania tumboni mpaka akatema damu ndipo wenzake walimshika mkono wakitaka atoke ulingoni lakini aligoma kisha akajipanga upya kumkabili yule muasi , muasi alijiandaa kumchoma yule mwanajeshi wa team rhino kisu ili naye apate wa kufa nae yule mwanajeshi alimkwepa kwa kuruka juu kisha muasi akapitiliza akamuongezea na teke la mgongoni lililomfanya apepesuke mpaka kwenda na kuanguka chini jambo lililowafanya wanajeshi wengine wa team rhino wamuamushe pale chini na kumsukumiza ndani ya duara ili aendelee kupigana ‘’zama ndani we mbwa upate haki yako si hutaki kusalenda’’ ilikuwa ni sauti ya mwanajeshi wa jeshi la Tanzania . Kichapo kiliendelea aliporudi tu ulingoni alikutana na ngumi za fasta fasta zilizomfanya azidi kuyumba , jambo ambalo lilimpa nafasi mwanajeshi wa team rhino kurudi nyuma na kukimbia kwenda mbele kisha kuachia ngumi nzito iliotua juu ya uso wa yule muasi kilichosikika ni kishindo cha mtu kudondoka chini na kupoteza fahamu pale pale.
‘’Team wolf team wolf narudia over’’ ‘’tunakupata tunakupata over’’ ‘’misheni inayofuata ni kuingia katika jengo walilomo mateka ili kumaliza misheni mapema over’’ ‘’tumekukopi over’’. Team wolf waliianza misheni ya kuelekea katika jengo waliloko mateka walipofika kwa nje kulikuwepo na waasi wawili waliokuwa na wasiwasi mkubwa kwani habari ya kuwa kambi imeisha shambuliwa walikuwa nayo , team wolf hawakuwa na papara walirusha bomu la machozi mahali walipokuwa waasi wale na kuwafanya waanze kukimbia hovyo nao wolf hawakutaka kuacha ushahidi waliacha risasi mithili ya njugu kuwafyekelea mbali wale waasi wawili waliokuwa pale langoni ili kazi ya kuwatoa wale mateka mule ndani ifanyike chapuchapu bila kupoteza muda kwani kama ingetokea waasi wameita back up team isiwakute pale.
Walizama mpaka mule ndani na kumkuta general akiwa miongoni mwa wale mateka walimpigia saluti haraka haraka na kuwachukua mateka wote ikiwemo kikosi kizima kilichokuwa na general team alpha haraka haraka general alitoa plani kwa kikosi chake kisha akauliza ‘’mmemaliza kambi yote’’ ‘’ndio mkuu’’ ‘’haya nipe redio call niite back up ya kuja kutuchukua’’ ‘’sawa mkuu hii hapa’’ yalikuwa ni maongezi baina ya sergeant danny na general wetu. General aliichukua redio call kisha kubonyeza namba za kuita usaidizi ‘’General Daitus misheni kuokoa mateka Nigeria kwa line mnanipata’’ ‘’Liutenant Mike wa team Omega ndio tunakupata mkuu over’’ ‘’Leta helikopta kutuondoa kwenye eneo la tukio misheni ishaisha over’’ ‘’dakika kumi tutakuwa tumeisha fika mkuu over’’ ‘’nimewakopi tutawawashia moshi wa rangi ya pinki ndani ya dakika tisa over’’ . Baada ya maongezi yale waliianza safari ya kutoka katika kambi ya waasi na kuingia msituni ambapo waliwasiliana na team zote na kukutania sehemu moja ambapo namimi nilikuwa miongoni mwao tukiwa tunasubiri helikopta ya kuja kututoa eneo la tukio. ‘’Sergeant danny washa moshi wa pinki kuwaelekeza mahali tulipo’’ ‘’ndio mkuu’’ ilikuwa ni amri ya General baada ya kusikia mlio wa helikopta juu angani, Sergeant Danny aliwasha moshi wa pinki eneo lile na ukatanda kwenda angani ambako ndiko hasa waliopo juu walitakiwa wauone moshi ndipo wateremke kuja kutuchua.
‘’General moshi wenu ni wa rangi gani mbona kuna moshi mwingi huku angani over’’ ‘’moshi wetu ni wa pinki over’’ ‘’Mkuu kuna moshi wa pinki mwingi huku angani sa tunashinndwa kuutambua moshi wenu tafadhali haraka haraka washeni mwingine tena over’’, bila hata ya kujibu General aliwasha moshi wa rangi nyingine raundi hii wa kijanii ‘’haya huko angani nimewasha moto wa kijani sijui mnauona over’’ ‘’mkuu moshi wote umebadilikaa kuwa wa kijani ni nini kinaendelea huku juu kuna moshi wa aina nane hivi tunashindwa kuelewa mbona imebadilika rangi kwa pamoja’’ ‘’hell shitiii!!! Kuna mchezo tunachezewa hapa’’ General alisikika akisema hivyo kwa hasira huku akionekana amechanganyikiwa kabisa.
JE NI NINI KINACHOFANYA MOSHI WA KUTOA SIGNAL UWE MWINGI ANGANI BADALA YA MMOJA NA UBADILIKE RANGI NA KUFANANA NA ULE WA WANAJESHI WA WATANZANIA???
ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU INAYOFUATA KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH