Mbinu 6 zitakazo kujenga katika mapishi yako



Moja ya jambo muhimu sana kwa mtu anaependa kupika vyakula vizuri ni ubunifu. Kwaiyo kama unaependa kuwa mtu unaepika chakula kizuri basi zingatia zaidi katika ubunifu wa mapishi maana mara nyingi ubunifu katika kukipika chakula ndio huwatofautisha wapishi na kuamua nyupi ni bora zaidi na kama ni mama wa nyumbani basi tambua kuwa mapashi ya kibunifu yanaweza ifanya familia ikifurahie chakula na kujenga afya pia. Tukiachana na maswala ya ubunifu, hapa tumekuandalia mbinu au mambo unayoweza kuyafanya ili kurekebisha mapishi yako yanapokua vibaya au kurahisisha upishi wako.

Mbinu 6 zitakazo kujenga katika mapishi


1. Mchuzi ukizidi Maji na kuwa mwepesi, kwangua kiazi mviringo kwenye kikunio cha nyanya weka katika mchuzi wako ili kuufanya uwemzito.



2. Chumvi ikizidi kwenye chakula weka kiazi mviringo kilichomenywa katika chakula ili kupunguza chumvi.



3. Laza maharage kwenye chupa ya chai yenye maji ya moto kisha asubuhi chemsha kwa dakika 30 tu yatakuwa tayari yameiva (yataiva haraka)




4. Ukimaliza kuosha vyombo kwa kutumia Still Ware,itunze still ware kwa kuiweka kwenye Maji ili isiharibike na ifae kwa matumizi ya kesho.




5. Ukiunguza wali kata kitunguu maji nusu kisha weka kwenye wali na ufunike kwa dakika tano. Kitunguu maji kinasaidia kutoa harufu ya moshi


6. Mchuzi wa maini ukitaka uwe rost nzito au mchuzi wowote na hauna nyanya za kutosha... Weka kijiko kimoja cha chakula cha unga wa ngano ukoroge na maji kidogo alafu weka kwenye mchuzi kisha acha uchemke dakika 5






Previous Post Next Post