Mnamo 1956, shirika la ndege la Grumman lilikuwa likijaribu ndege mpya ya mapigano iitwayo F-11 Tiger, karibu na pwani ya jimbo la New York.
Ndege ambayo ilikua inanafasi ya kukaa ya mtu mmoja tu. Lengo kubwa la kutengenezwa kwa ndege hiyo lilikua ni kuitumia katika shuguli za vita vya anga hivyo ndege hiyo ilikua ya kivita.
Rubani aliondoa dege hiyo aridhini na kuipandisha juu Kisha baadae alifyatua risasi toka kwenye ndege hiyo kuelekea mbele na muda mfupi baadaye aligundua ndegeyake imepata uharibifu kwenye kioo cha mbele na kwenye injini.
Nini kilitokea?
Rubani alipokua angani alikua kasi sana na alipofyatua risasi mbele, ndege ilikutana na risasi hizo kabla hazianza kushuka chini. Kwa namna nyingine tunaweza sema ndege hii ilikua na kasi kuliko risasi angani mpaka ikaweza kujipiga risasi yenyewe.