MTUNZI: CLEMENT CHARLES A.K.A COWBOY KING
........."Pakini mizigo yenu na tuianze safari mara moja", ilikuwa ni sauti ya lieutenant mike ambae alipewa order na brigedia Pele ili tujipange kwa ajili ya safari ya kuelekea porini nchini Nigeria ambako tunapelekwa ili tukatoe msaada kwa wahanga na mateka waliokamatwa na kikundi cha Waasi. Nikiwa napaki mizigo yangu niliyakumbuka maneno ya baba aliyoniambia kuwa nipigane ili kuijengea heshima nchi yangu na nihakikishe ninarudi salama, na nikashika shingoni mwangu kuangalia cheni iliyofanyiwa matambiko na wazazi wangu nikaikuta ipo nikapiga moyo konde na kujipa matumaini kuwa nitarudi salama.
Tulianza kuisombea mizigo yetu kwenye ndege kubwa iliyokuwa imefika pale kwenye uwanja wa kambi ya jeshi kwa ajili ya kutuchukua na kutupeleka nchini Nigeria ambako vita vinapamba moto kati ya makundi matatu, serikali iliyopo madarakani, waasi na kikundi cha waislamu wenye imani kali boko haramu.
Tulimaliza zoezi la kupakia kisha nasi tukaingia ndani ya ndege ile kisha tukafunga mikanda, Mara injini ziliunguruma na kuanza kuiacha ardhi ya nyumbani kwa kasi kisha tukapaa angani, kwa kweli ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda ndege kwenye maisha yangu ya kijeshi japo tulikuwaga tunajifunza jinsi ya kuruka na parachuti kwa kutumia majengo marefu na helikopta ndio ujuzi pekee nilionao pamoja na kulenga shabaha za masafa marefu kwangu haikuwa shida hata kidogo.
Nilishituliwa na sauti ya rafiki yangu nilie nae team moja sergeant Hashim "sergeant Gedi mkuu anaingia acha kuwaza". Tuliamka kwa haraka na kwa upamoja tukampa saluti kama ilivo ada kwa wanajeshi kumpa saluti mtu anaekuzidi cheo.
Aliitikia salamu zetu kisha akatuamuru tukae chini kisha akaanza kutuambia kuwa " Tumebakiza masaa mawili tuingie nchini nigeria, na kazi iliyotuleta hapa ni kupambana na waasi wa serikali sawa" tuliitikia "sawa mkuu" kisha aliendelea "Ramani ya mahali tunapoenda kuvamia na kuianza mission(misheni) hii hapa"", tulipitishiwa ile ramani kila mmoja kisha tukatikisa vichwa kuwa tumeielewa kabisa.
Mkuu alitoa agizo akisema "hapa kuna team nne nilizopanga ambazo ni team alpha ambayo itaongozwa namimi mwenyewe, team wolf ambayo itakuwa chini ya sergeant danny, team rhino ambayo itaongozwa na Sergeant gedi, na team omega ambayo itaongozwa na lieutenant mike". General baada ya kuyasema hayo makundi alivuta pumzi tena kisha akaendelea " team wolf na team rhino tutawaacha katika kijiji hiki ndipo mtatulia na parachuti zenu kisha team wolf utachukua njia ya kama kuelekea mashariki ili kuifikia kambi ya maadui na team rhino utaelekea magharibi, kisha Mimi na team omega tutakuja kwa upande mwingine wa msitu ili kumweka adui katikati tumeelewanaa"" tulijibu "ndio mkuu" kisha akamalizia kwa kusema "mjichunge Sana kwani Nigeria ni nchi ya hatari sana kwani kuna kundi hatari la boko haramu, tumieni mbinu zote za kijeshi kuhakikisha kuwa tunarudi wote salama na msijaribu kugusa vitu hovyo muwapo msituni"
Ulipita muda kama wa nusu saa ndipo general alipoongea tena "haya vijana wa team wolf na rhino jiandaeni kwa kuruka", tulichukua mabegi ya silaha zetu tukafunga vyema na parachuti zetu tukaelekea mlango wa nyuma kwa ajili ya kujiachia hewani.
Je,team rhino na team wolf watatua salama kwenye nchi ya Nigeria???
ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU YA PILI KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH