Bwana mmoja aliota ndoto amemtalaka mkewe,akaenda kwa kadhi na kumsimulia juu ya ndoto yake,yule kadhi akamwambia yule bwana ni sharti amuache mkewe. Yule bwana akamuacha mkewe,baada ya siku si nyingi yule kadhi alimuoa yule mwanamke,yule bwana alisononela sana kwa kua bado alikuwa anampenda mkewe. Hivyo akamueleza kisa chote Abunuwasi,alichokifanya Abunuwasi alikodi watu na kwenda kwenye nyumba ya yule kadhi na kuwaambia wale watu aliowakodi waanze kuvunja ile nyumba. Kazi ya kuvunja ile nyumba ilianza,kadhi na watu walipohoji ni kwa nini Abunuwasi anafanya hivyo,akasema ameota kwamba baba yake alimuwachia hazina ya mali na imchimbiwa sehemu ilipo nyumba ya kadhi,watu walipohoji tangu lini ndoto ikawa kweli? Abunuwasi akawajibu tangu huyu bwana alipoota kuwa amemwacha mkewe na kadhi akasisitiza huyu bwana shurti amuache mkewe,hapo ndipo ndoto inakuwa kweli