Nadhani umecheza game nyingi sana katika mwaka 2020 na natumaini unaendelea kufurahia mambo mazuri kuhusu games kupitia app yako ya Traah. Sasa huu ni mwaka mwingine na nakwenda kukujuza kuhusu baadhi ya magame makali na yaliobora ambayo unaweza kuyacheza mwaka huu wa 2021 na yakakufurahisha.
1. Overkill 3
Hili ni game zuri sana la Action ambalo mpaka sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 5. Linamuonekano mzuri na watu wengi wanalipenda kutokana na muonekano wake wa kipekee kidogo.
Game hili huchezwa bila data (Offline) pia linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja kwa kutumia data (Online).
Inashauriwa anaecheza game hili awe na miaka 16 na kuendelea.
Overkill 3 ni game lipatikanalo Playstore kwa MB 401 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
2. Takashi Ninja Worriror: Shadow of last samurai
Hili ni moja ya magame mazuri sana ambayo kwa sasa yako trend katika playstore. Game hili ni la kijapani na linamuhusu kijana Takashi ambae anaingia katika kulipa kisasi kutokana na watu wake kufanywa vibaya.
Ukilipakua utaweza kulicheza muda wowote na bila kukugharimu chochote maana game hili huchezwa bila data (Offline) pia hupatikana kwa MB chache sana zisizopungua MB 87.
Unaweza kulipata kirahisi katika playstore kwa kugusa INSTALL
3. Modern Strike Online
Ni moja ya magame bora ya kivita ambayo huchezwa Online tu. Limechezwa na watu wengi sana wasio pungua Milioni hamsini(50).
Game hili ni moja ya magame yanayofanana na game la Call of duty hivyo kama unapenda magame ya jamii ya Call of duty, usiache kucheza game hili.
Katika game hili unaweza cheza na marafiki zako Online kwa kiunda timu ya kuwaangamiza maadui au mukashindana kuua maandui ili atakaewaua maadui wengi awemshindi.
Modern Strike Online ni game lipatikanalo Playstore kwa MB zisizopungua MB 494. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
4. Zombies Rait
Ni game la Zombies ambalo likovizuri mpaka linatisha. Zombies Rait ni game lililotengenezwa Urusi ambalo linamuhusu mwanajeshi aliebaki mzima katika vita ya pili ya dunia lakini ghafla ananza kupigana na wenzake waliokufa ambao wapo katika hali ya kizombie(Wafu wanao tembea). Limetoka mwisho wa waka 2020
Linamazingira yanayotisha pia Zombies wake wapo vizuri sana ukifananisha na wamagame mengine. Lugha ya game ni kirusi lakini game linaeleweka.
Game hili ni zuri sana na linapatikana playstore lakini si bure. Linauzwa Shiringi 2200 tu. Unaweza kulipakua kwa kugusa INSTALL
5. Real Moto
Kama ni wewe ni mpenzi game za mashindano ya pikipiki basi real moto linaweza kuwa bora sana kwako. Game hili huchezwa bila kutumia data yaani ni game la Offline. Limechezwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10).
Utaweza kutunza kumbukumbu zote za game hilo kwenye email yako ili simu ikipotea uendelee kucheza palepale ulipoishia kucheza game hilo pindi utakapopata simu nyingine na kuiingiza email yako.
Game hili hupatikana playstore kwa MB 143. Unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
6. Garena Free Fire
Garena Free Fire linatumia data na lipo hivi; Unamchagua mtu wako utakaemchezesha kisha unatupwa katika eneo moja na wenzako 49 wanaocheza game hilo muda huo duniani ili mupigane na uwemzima. Kwaiyo kila mtu utakaemuona katika game hili ni mtu anaepambania maisha na anaecheza game kama wewe.
Zaidi ya watu Milioni 500 ulimwenguni wanalicheza game hili kupitia vifaa vyao vya Android. Ni game linalopendwa na watu wengi kutokana na kuwa dogo kuliko magame mengine ya muundo huu ambayo ni UBUG na CODM.
Unaweza kulipakua katika playstore kwa MB 674 pia unaweza rahisisha upatikanaji wake kwa kugusa INSTALL
7. Rarry Fury: Extrime racing
Kama unapenda magame za magari usiache kupakua game hili lenye utofauti mkubwa na magame ya magari yanayotamba kila mwaka. Game hili ni moja kati ya magame yanayopendwa na watu na mpaka Sasa limepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 50. Linauhalisia wa kufurahisha wa mashindano ya Rarry.
Ukiachilia mbali muonekano wa game hili kuwa mzuri pia game hili linawezwa chezwa na mtu mmoja Offline au zaidi ya moja Online.
Lina MB 120 na linapatikana katika playstore pia unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
8. eFootball pes 2021
Ukiongelea game kali za mpira wa miguu katika mwaka 2021 huwezi acha game hili. Game hili limepakuliwa na watu wengi sana hapa duniani na hii ni kwasababu liko vizuri.
Linachezwa Online na inashauriwa kuwa na mtandao usiosumbua ili uweze kulifaidi game hili bila usumbufu.
Hupatikana playstore kwa GB 1.6 pia unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
9. Real Boxing
Hili ni game la mchezo wa ngumi ambalo mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 10 ulimwenguni. Lipo vizuri sana kwanzia muonekano hadi sauti za vitasa(Ngumi).
Kama ni mpenzi wa magame ya kupigana, usikubali kuliacha game hili maana ni game lenye uhalisia wa mchezo wa kupigana wa Boxing.
Inashauriwa anaecheza game hili asiwe na miaka chini ya kumi na sita (16+).
Game la Real Boxing hupatikana playstore kwa MB 291 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
10. Jumanji: Epic run
Kama unaijua vizuri filamu ya Jumanji au game la Tempo Run basi unaweza kulipenda zaidi hili game maana limeundwa kutokana na filamu ya Jumanji na muundo wake unafanana na game maarufu liitwalo Tempo Run.
Ni game ambalo hujezwa bila data na mpaka Sasa linachezwa na zaidi ya watu million 10 duniani. Mchezaji wa game hili anatakiwa kuwa na umri usiopungua miaka 12.
Linapatikana playstore kwa MB 154 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL