1. Weupe wa penzi lako ni kama mwezi angani.Ucheshi na mahaba yako huwa sijui nifananishe na nini? Kupata mfano wako hakutokea milele. Elewa mimi ni wako na moyo wangu nimekupa wewe.
2. Mpenzi kila siku waniahidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hufikilii kuwa ahadi zako huniniumiza pindi unapoamua kutotimiza. Plz badilika ... Nakupenda.
3. Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika na amini kuwa wewe ndie mwanamke peke ambae moyo wangu umeuteka. Nakupenda Sana.
4. Nimetumia muda mwingi kuzunguka pande zote za Tanzania macho yakiangaza kumsaka wa kunivutia na kunifaa. Hatimae mungu kanikutanisha na wewe, ndoto yangu imetimia.
5. "Mimi na wewe basi, Sikupendi, Sikuhitaji na Sitaki unifuate tena" Ni baadhi tu ya maneno ambayo sitamani kabisa sikumoja yatoke midomoni mwetu maana huumiza. Tukumbuke kulinda penzi letu usisikilize kelele. Kwa upande wangu nakuahidi nitakupenda milele na moyo wangu wote unao wewe.
6. Sijui nikuekleza namna gani uelewe yaliyionijaa moyoni kwani kila nifikiriapo kwanini una walakini na hutaki kuniamini kama wewe pekee ndiye ninayekupa mahaba yangu makini, mpenzi rudisha yako imani ni wewe pekee nayekupenda hapa duniani!
7. Naweza kukushangaza ila tambua mimi si wa kwanza. Japo ni mwanamke, ninahisia na nimeshindwa ficha zangu hisia. Moyo wangu na akili zangu zimekwama kwako. Tafadhari nielewe nakupenda mwenzako.
8. Naamini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi, tafadhali badili yako mavazi , bafuni ingia upate maji kujimwagia, natamani kuja kukusaidia mgongo kuusugua na chakula kukuandalia lakini siku haijawadia, nakupenda dear!
9. Kwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa usoni, busu la amani hubusiwa mashavuni, busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la mapenzi hubusiwa shingoni, Je wapi nikubusu ili ulale kwa raha usiku wa leo sweet ?