Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini?



Simu kuingia maji Ni moja ya mambo ambayo hutokea katika shughuli zetu za Kila siku. Jambo hili huogopesha sana maana husababisha mpaka baadhi ya simu kupata matazizo au kutowaka kabisa. Hatuwezi zuia simu zetu kuingia katika maji maana hutokea Kama ajali, lakini tunaweza zuia simu zibaki salama yaani zisiwe na matatizo yoyote baada ya kuingia kwenye maji.
Kama simu yako imeingia maji na unahitaji iwesalama basi fanya mambo yafuatayo;


1. Zima simu



Baada ya simu kuingia maji unatakiwa kuhakikisha aiendelei kuwaka. Izime bila kupoteza muda maana ikiendelea kuwaka maji yalioingia yatasababisha vitu vya ndani ya simu hiyo kuharibika.

2. Chomoa betri



Kama simu yako inachomoka betri hakikisha unachomoa betri na kuliweka pembeni ya simu ila kama simu yako si ya kuchomoka betri, Fanya kuichoma line au memory Kisha kimbia moja kwa moja kwa fundi ili ifungue na kutenganisha muunganiko wa betri na simu kabla ya kuiacha ikauke

3. Iachewazi katika sehemu kavu


Chomoa line ya simu,Memoy na ikiwezekana nenda kwa fundi aliopo karibu na wewe ili aifungue ibaki wazi na kukauka kirahisi. Baada ya kuiweka wazi unatakiwa kuiweka sehemu kavu kwa muda mrefu mpaka itakapokauka kabisa.




Zingatia: usijaribu kuiwasha simu kwa kuijaribu kabla ya kufuata hatua hizi!



Ukweli kuhusu mchele: Watu wengi huweka simuzao katika mchele wakiamini simu zao zitapona lakini kitu cha muhimu kukijua ni kwamba, mchele ni unaweza kukausha maji tu hivyo kabala ya kuweka huko unatakiwa kufuata hatua hizi pia.




Kama itakua si maji ila vimiminika vingine: kama simu itangia katika pombe,Maji ya chumvi na vimiminika vingine, utatakiwa kuzima na kutoa betri kisha Kifungua nakuisafisha au kuifuta na kitambaa maana usipofanya hivyo baadhi ya vimiminika vikikaukia ndani ya simu, huozesha baadhi ya vitu vilivyo ndani ya simu (ukishindwa ni bora upeleke kwa fundi).

Simu ilioathirika kutokana na mtumiaji wake kutofuata hatua hizi muhimu baada ya simu yake kuingia maji.




Previous Post Next Post