Agano: 06 (Simulizi)





MTUNZI: CLEMENT CHARLES


INAENDELEA;
…….Nilidondoka kutoka juu ya mti mpaka chini puuh!! Jambo ambao liliwafanya wanajeshi wote na mateka washituke na kujiweka sawa kwa aina yoyote ya uvamizi itakayojitokeza mahala pale na General aliwaagiza wanajeshi wenzangu wawili kuja kuniangalia pale nilipoangukia na kunikuta nikiwa nimepoteza fahamu ‘’mkuu tunaona yuko sawa anapumua ila kapoteza fahamu tu’’ ‘’mleteni huku kisha mmoja abakie hiyo nafasi yake kuangalia usalama’’ ‘’sawa mkuu’’, walinisogeza hadi maeneo waliyokuwa wamekaa wale mateka na wanajeshi wengine kwa ajili ya kupumzika na kuniweka pale kujaribu kuangalia njia nyingine ya kunizindua.
Nikiwa katika usingizi mzito ule uliosababishwa na kuzimia kwangu nilianza kuota ndoto ambayo ilinistua sana , (maisha ndani ya ndoto wakati nikiwa nimezimia) nilijikuta nikiwa na nimevaa shuka jeupe ndani ya ndoto ile huku nikiwa na ile cheni shingoni shingoni huku mkononi nikishikilia gongo lililokuwa likinisaidia kupanda mlima ambao juu yake kulionekana kufuka moshi mweupe mithili ya seruji la barafu niliendelea kukipanda mlima ule lakini cha kushangaza zaidi kulikuwa na sauti za watu chini ya mlima ule wakilia na kuomba misaada ‘’Gedi ukiinuka inuka nasisi kaka’’ ‘’wewe ndo mwokozi wetu kwa sasa’’ ‘’usituache tukaangamia huku nigeria’’ , zile sauti ziliendelea kuuchanganya ubongo wangu na nikabaki katikati ya kilima nikashindwa kupanda wala kuteremka huku sauti za watu wale zikinijia kichwani mara mbilimbili wakati nikiyafikiria hayo nilisikia sauti nyingine ikitokea katika kilele cha mlima ikisema ‘’Ukitaka kuziokoa nafsi zisizokuwa na hatia ndani ya msitu huuu na urudi nchini Tanzania lazima ukubalie nasi katika AGANO lenye masharti’’ nafsi ilizidi kuingiwa na woga na kunifanya nirudi hatua moja nyuma kwanza huku nikifikiria kichwani ‘’agano ndio nini mbona sielewi’’ wakati tena nikiyafikiria hayo nilihisi sauti ikininong’oneza masikioni ‘’kubali hilo agano mjukuu wangu hayo ni mambo ya mizimu na huenda mizimu ya huo msitu imekupenda’’ tena baada ya hapo maneno yale yalianza kujirudia masikioni mwangu yakisema ‘’kubali hilo agano mjukuu wangu’’ ‘’kubali hilo agano’’.
‘’Hapana’’ nilishituka kutoka katika ule usingizi mzito (kuzimia) na kumkuta general akiwa karibu yangu akivipasha viganja vyangu joto ‘’sergeant tulia kwanza tatzo ni nini’’ ‘’mkuu nini kilitokea’’ ‘’ulianguka kutoka juu ya mti ndo tukawahi kukuokota we pumzika kwanza afu tutaangalia utaratibu mwingine’’ ‘’sawa mkuu’’, kwa vile general aliniamuru nilale nami nikalala na tena akaongeza robo saa ya kupumzika ili tu kuhakikisha narudi sawa ‘’nimeongeza muda wa kupumzika dakika kumi na tano mlioko lindo badilishaneni na hawa waliokuwa wamekaa’’ ‘’sawa mkuu’’ baada ya kupokea amri ile mpya watu walibadilishana nafasi mara moja.
Wakati nikiwa katika usingizi ule wa pili nilianza tena kuota ndoto nyingine ‘’ nilifika katika kilele cha mlima ule na kumkuta mzee mmoja mwenye umri wa miaka tisini akiwa anaweka vitu kama majani ya mgomba kwenye pipa la chuma kufanya moshi mzito mweupe utoke katika lile pipa, nilipofika pale nilimsalimia ‘’mzee shikamoo heshima yako’’ ‘’marhaba gedi kutoka Tanzania nchi yenye amani na utulivu wa hali ya juu’’ ‘’mzee umenijuaje jina langu’’ ‘’we ni kipenzi cha mizimu nitaacha kukujuaje kijana uliestaarabika’’ ‘’haya mzee mimi nimekuja huku kufanyeje’’ ‘’umekuja huku kufata msaada kwa ajili yako wewe na wanajeshi wenzio koh inabidi utulie na unifuate’’ ‘’sawa mzee wangu’’. Nilianza kuongoza njia kumfuata yule mzee alienda na kuketi kwenye jiwe name akaniita nikaenda kuketi nae karibu ‘’sasa kijana ukitaka kutoka salama katika huu msitu unatakiwa ufuate mambo yafuatayo’’……..

JE NI MAMBO GANI HAYO GEDI ANATAKIWA AYAFUATE?

ENDELEA KUFUATIA SEHEMU INAYOFUATA KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH
Previous Post Next Post