Kubusu ni kitendo kinachohusisha hisia ambacho wapenzi hujikuta wanafanya lakini nia huwa ni kuonesha upendo na ndiomaana kunakua na ugumu kidogo katika kumbusu mtu ambae haumpendi au hakupendi.
Katika mapenzi kilakitu huwa na sababu na vile vile huwa na faida. Busu limeonekana kuwa na faida nyingi kwa washiriki wa kitendo kicho. Hapa nakupa faida 5 tu za busu (busu la mdomo kwa mdomo) na faida hizo ni zifuatazo;
Faida za busu
1. Busu huboresha tendo kati ya wapenzi
Ikiwa wajua kubusu basi utakuwa na uwezo wa kufurahia tendo na kumfurahisha mwenza wako pia kwa sababu busu huchangia kwa kiasi kikubwa katika kumfanya mtu awe na hisia nzuri katika tendo. Watu wengi hupuuzia kitendo cha kubusu lakini kinamchango mkubwa sana na hakikisha unajua namna gani ya kumbusu mwenza wako kwasababu ukiwa unabusu hovyo hovyo unaweza mkera mwenza wako kila siku na kamwe hawezi kukwambia ukweli kuwa hujui kumbusu.
2. Busu litakufanya uwe na furaha
Kama umekuaukijiuliza kwanini huwa unafurahia kupiga busu basi leo tambua kuwa kile kitendo tu cha kupiga busu huwa ni chanzo cha furaha.
Wataalamu wamebainisha kuwa kumbusu mpenzi wako au kushiliki tendo kunasababisha mwili kutoa homoni ya oxytocin ambayo humfanya mtu kuwa na furaha.
3. Busu hupunguza kuumwa na kichwa na maumivu ya hedhi
Hii ni nzuri haswa kwa wanawake wanaoumwa na kichwa na wanaougua maumivu ya hedhi. Kwa hiyo wakati mwengine unapoumwa na kichwa, maumivu yanaweza kutulia endapo utakutana na mpenzi wako na kumpiga busu au kushiriki nae tendo.
4. Huimarisha afya ya meno
Kama huwa unambusu mpendwa wako kisawa sawa utagundua pindi unapokua katika kitendo cha kubusu, mate huongezeka kwa kiasi kikubwa mdomoni.
Mtu hudondokwa na mate zaidi anapobusu na hiii husaidia kusafisha meno na kuyakinga na uozo unaotokana na mabaki ya chakula
5. Hupunguza msongo wa mawazo
Kama tunavyojua kuwa msongo wa mawazo unaweza kuwa na athari kubwa katika maisha yetu lakini ningependa ufahamu kuwa kubusu huwafanya wapenzi kusahau matatizo wanayopitia pia huufanya moyo kusukuma damu pande zote za mwili.