"Ahaa Jimmy... Ndio ninachokupendeaga Shem langu huchoki kuniungisha" Ilikua ni sauti ya Sophia akimkaribisha Jimmy pindi alipokua anaingia.
"Hahaha hapa ndio nyumbaniii nikipachoka hapa nitaenda wapi sophi?" Jimmy
"Hahaha ni kweli kabisa shemeji yangu... Karibu uketi" Suzi
"Asante" alisema Jimmy huku akiaa katika kiti kilichokua karibu kabisa na jikoni ambako Sophia alikua akipika na muda huo kulikua hakuna wateja zaidi yake. "Enhe nikupe nini leo?" Sophia alimuuliza Jimmy na Jimmy akajibu"Kama kawaida yangu... Wali Nyama ila leo pilipili sitohitaji kabisa"
Sophia jibu sawa kisha akaita kwa nguvu "Nuruuuuu!!!!" ikaskika sauti ya binti akiitika toka nje ya kibanda hicho kidogo cha magahawa wa Sophia. Binti huyo Ni mfanya kazi mpya wa mgahawa huo na aliitwa na Sophia ili amuhudumie Jimmy kwa kumpelekea chakula. Nuru alifika ndani ya mgahawa na akawa anapewa maelekezo juu ya kumuhudumia Jimmy ambae alikua akisubiri chakula muda huo huku akiwaza juu ya safari ya kwenda kwa mrembo Suzi kuijaribu bahati yake.
Kabla hata chakula hakijaletwa mezani kwa Jimmy iliskika simu kikiita mfukoni mwa Jimmy. Moyo wa Jimmy ulidunda kwa furaha kwakua alihisi anaempigia ni Suzi maana muda waliokubaliana ulikaribia Sana na zilibaki dakika 40 tu kufika saa 8 kamili hivyo alipeleka mkono mfukoni na kuitoa simu huku akitupia vijicho vya kuzuga kwa Sophia ambae humuita shemeji kutokana na kua na urafiki mkubwa na Rose.
Lakini ghafla alipoteza furaha kabisa baada ya kukuta jina la aliekua akipiga limeandikwa "MWENYE NYUMBA" kwakua mwenye nyumba amekua akimdai Kodi ya miezi minne na siku hiyo Ilikua ni siku waliokubaliana kuwa Jimmy atailipa Kodi lakini ukweli ni kwamba Jimmy hana mpango wowote wa kulipa Kodi hiyo kutokana na mambo yake kwenda vibaya kila siku japo huwa hakosi hela ya kula.
Jimmy aliirudisha simu hiyo mfukoni huku ikiendelea kuita mpaka ikakatika. Mwenye nyumba hakukata tamaa alipiga simu tena mpaka Jimmy akaamua kuifunga simu yake sauti ili kuepukana na kelele. Baada ya dakika chache Jimmy aliletewa chakula mezani na binti Nuru ambae ni binti mdogo mdogo lakini yupo vizuri kimuonekano hasa kifua kilikua kimesimama mpaka kikamfanya Jimmy alopoke kwa sauti na kumuuliza Sophia "Duh ivi Sophia umemtoa wapi huyu binti?" huku aliendelea kula wakati Nuru akitoka nje.
"Hahaha utaka kumsaliti rafiki yangu Rose eehe?" Sophia alimwambia Jimmy
"Hahaha siku moja moja sio mbaya au unaonaje Shem?" Jimmy alijibu kiutani tu
"Haha wanaume bwana.. Sasa si bora utoke na mimi mkubwa mwenzio kuliko hako katoto" Sophia alimwambia Jimmy
"Hahaha inamana na wewe unataka kamsaliti rafiki yako?" Jimmy alimwambia Sophia huku aliendelea kula chakula.
"Mh kwa uhandsome huo... Nashindwaje kwa mfano? Ni wewe tu.. nakupa ushike popote utakapo hahahaha" alisema Sophia kwa aibu na sauti ya chini kidogo akiwa kama anatania vile lakini ukweli ni kwamba huwa anamtamani Sana Jimmy ila huwa anashindwa aanzie wapi kumueleza Jimmy maana Jimmy ni mpenzi wa rafiki yake hivyo huishia kumuonesha upendo wake kwa kumpa chakula bure mara kwa mara.
Jimmy na Sophia waliishia kucheka tu "hahahaha" na wala Jimmy hakugundua kuwa Sophia amezielezea hisia zake za kweli kwa njia ya utani...
Mwisho Jimmy akamaliza kula na alipotaka kulipia chakula, Sophia hakutaka kupokea malipo ya Jimmy kwa kudai kua ni Shemeji wa karibu sana hivyo atalipa hata siku nyingine lakini ukweli ni kwamba Sophia anadhani anaweza mpata Jimmy kwa kumfanyia hivyo na hujipa moyo kuwa "IPO SIKU ATANIELEWA... LAZIMA ATANIELEWA!"
UNAFIKILI PENZI LA SOPHIA LITAPATA VIPI NAFASI KATIKA MOYO WA JIMMY IKIWA ROSE MWENYE AMEBAKIZWA JINA TU?
ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU INAYOFUATA KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH...