Abunwasi alikuwa na mpwa wake yaani mtoto wa Dada ake ambaye alikuwa anaishi kitongoji tofauti na abunwasi. Mpwa wa abunwasi aliishi jirani na mtu mmoja tajiri, mpwa wa abunwas hakuwa na uwezo sana hapo naamanisha kipato kidogo ambacho hawezi kula chochote atakacho. Siku moja mpwa wa abnwasi baada ya kutoka mihangaikoni akapika ugali akawa hana kitweweo kabisa wakati àkiwaza atpataje kitoweo jirani yake ambaye ni kwa yule tajiri wanatayarisha nyama sasa kwa maandalizi bab kubwa na viungo ile nyama ikawa inanukia kwelikweli, basi mpwa wa abunuwasi kutumia ile haruu akala ugali wote kwa kutumia ile harufu kama kitoweo, siku inayofuata akamfata tajiri na kumpa shukran kuwa harufu ya nyama yake ilimsaidia kwani alitumia kama kitoweo katika chakula chake, basi yule tajiri alifula mbaya akasema haiwezekani akala ugali kwa kutumia harufu ya nyama yake ndo mana nyama yake haikuwa tamu, akamfungulia kesi mahakamani. Kwa sababu mpwa wa abunwas hakuwa na uwezo kipesa aliamua kumfuata mjomba wake amsaidie, basi siku ya kesi walienda mahakamani kesi ikasiilizwa na mahakama ikamkuta na hatia mpwa wa abunuwaskwani kunusa harufu ya ile nyama no sawa na kula ile nyama bila ridhaa ya mwenyewe, hakimu aliamuru tajiri alipwe fidia ya fedha kwa kukoseshwa utam kwenye nyama yake, tarehe ya kulpa faini ilipangwa basi abunwas alirudi nyumbani na mpwa wake, siku ya kulipa abunwas alibeba sarafu kwa kiasi chote cha pesa alizopaswa kulipa, basi kufika court mshitakiwa akaulizwa fine umeleta akajibu mjomba atalipa kwa niaba yangu, mahakama ikamuru abunuwas atoe akabidhi kwa mlalamikaji, basi abunwasi alizipigisha chini zile sarafu zote, akauliza mmesikia sauti watu wote wakjibu ndio, akapiga tena na kuuliza kama watu wote wamesikia walijibu ndio tumesikia sauti, alifanya kitendo hicho Mara tatu, baada ya hapo akasimama na kusema kuwa tayari nimeshalipa fine kwa niaba ya mlalamikiwa hakimu akauliza kivipi abunwasi alijibu kuwa kunusa harufu ya nyama ni sawa na kula nyama yenyewe basi kusikia sauti ya pesa ni sawa na pesa basi mpwawe aliachwa huru! Tusamahane kwa mpangilio usio wa kihandishi