MTUNZI: CLEMENT CHARLES
INAENDELEA;
…….Nilichokiona ni tofauti na nilichoambiwa , badala ya kuona mti unaoyumbishwa na upepo niliwaona kina mama wawili wakiwa uchi wa mnyama wakiuzunguka ule mti mkubwa eneo lile tena huku wakiwa wameshika mikononi mwao kitu kama kiganja cha mkono wa binadamu wakiusontosha mbele yao wakati wakifanya ule mzunguko. Baada ya kuona jambo lile niliogopa lakini sikutaka kuonesha kama kuwa nimeogopa bali ilibidi nitoe amri kama kiongozi wa team Rhino ‘’Team Rhino tulieni hapo hapo mpaka pale nitakapowapa amri yangu over’’ ‘’tumekukopi sergeant over’’. Niliichukua tena darubini yangu kwa mara nyingine kuangalia nalisovu vipi tatzo lililopo mbele ya kikosi changu , nilipoangalia tena niliona wale wakina mama wakiwa wamewasha moto kwenye ule mti tena raundi hii wakianza kwa kuuchoma ule mkono kwenye moto mpaka ulipoungua kisha waliutoa na kuanza kuula kama mtu alae nyama ya kawaida, baada ya kufanya yote hayo mmoja wapo alitoka kama anaenda pembeni akarudi na vitambaa viwili kimoja akampa mwenzake nayeye akabaki na kimoja kisha walijifunga kichwani kushikana mikono na kutoweka katika mazingira ya ajabu ambayo hata mimi nilibakia nimeduwaa.
‘’Team Rhino hii ni Team Wolf mnatupata over’’ niligutuliwa na sauti ya redio kutoka katika kikosi cha pili cha team wolf kikiwa chini ya sergeant Danny ‘’Nawapata vyema kabisa vipi hali kwa upande wenu over’’ ‘’hali kwetu ni shwari na mpaka sasa tumefanikiwa kuingia upande wanakoweka silaha hawa waasi tunasubiri tu nyie mfanye ambushi afu sisi tuwashe moto hili ghala la silaha over’’ ‘’sawa nipeni dakika tano nikipange kikosi changu tayari kwa kuivamia kambi ya adui kirahisi sergeant over’’ ‘’tumekukopi sergeant over’’ . Niliinyanyua redio call yangu tayari kukipa maelekezo kikosi changu na kukiuliza ile hali ya mti kuyumba kama bado ilikuwepo maeneo yale nao wakanijibu imeisha niliwapa amri ya kusonga mbele huku wakiwa na tahadhari kubwa kwani wote tulikuwa wageni maeneo yale na ni operesheni ya kijeshi iliyotupeleka pale.
Niliishika tena kuiweka bunduki yangu ya masafa marefu tayari kuianza kazi ya kugawa dozi kwa wale waasi nilianzia pale nilipowauliwa wale wawili wa mara ya kwanza afu nikazidi kuzoom kuangalia sehemu ya ndani ndipo nilipoona kundi la waasi wakicheza na wanawake ambao nao walionekana ni waasi fika kwani nguo walizokuwa wamevalia zilikuwa ni za kijeshi kisha nilijaribu kuipeleka bunduki yangu pembeni ndipo nilipomuona mkuu wa waasi wale sikutaka kupoteza muda nilimweka kwenye tageti japo alikuwa akinywa kilevi, huku nikiivuta trigga yangu taratibu nilipobonyeza tu na kufyatua risasi nilitoa amri kwa vikosi vyote ‘’Team Rhino na Team Wolf fire’’ , ndipo kazi ilipoanzia kwani team rhino waliingia kwa kushitukiza huku wakiachia risasi mfululizo kuwapiga wale waliokuwa wakicheza pale bila huruma huku wakiwa waangarifu zaidi waliwashoot za kichwa kuhakikisha hamuna atakayeamka na kuja kuwasumbua tena.
Team Wolf nao hawakuwa nyuma waliilipua ile ghala ya silaha kwa kutumia grenade(bomu la mkono) na kuwafanya waasi waliokuwa wakikimbilia kule kwenda kujihami kwa kuchukua silaha ili wajibu mapigo wachanganyikiwe na kuianza safari ya kurudi walikotokea jambo ambalo team wolf hawakutaka litokee walitokea kwa nyuma huku wakiachia risasi na kurusha mabomu ya mkono kwa wingi na kusababisha moto uzidi kuwa mkubwa maeneo yale huku kelele za vilio zikizidi kutawala maeneo yale ilisikika tu lugha ya kiswahili na kinigeria ‘’piga ua mbwa haoo’’ ‘’iyoo iyoo ikemma is die yo am going to die with all of you’’ ilikuwa ni sauti ya mwanajeshi wa kikosi cha team wolf pia na sauti ya mwanajeshi wa kikosi cha waasi wa Nigeria aliyeshuhudia mwenzake akiuliwa mbele yake.
Sikutaka kuwa mbali na kikosi changu niliweka bunduki chini na kuchukua darubini kukiangalia niliwaona wanajeshi wa kikosi changu wakiwa wamezungusha duara kisha wakamuweka mwanajeshi wa waasi mmoja na mwanajeshi wa kitanzania tayari kwa ajili ya kupigana na tayari mwanajeshi wa waasi alikuwa na kisu mkononi …..
JE, MWANAJESHI WA KUNDI LA WAASI ATAFUA DAFU KWA MWANAJESHI WA TEAM RHINO?
USIACHE KUSOMA SEHEMU YA NNE KUPITA APP YA TRAAH.