Mazoezi yenye faida katika tendo la ndoa




Mazoezi ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa sababu huuweka mwili vizuri na huuepusha na baadhi ya magonjwa pia. Mazoezi pia yamethibitika kusaidia katika kuuweka mwili mwili vizuri katika upande wa tendo la kujamiiana/kufanya mapenzi kwa jinsia zote mbili. Lakini unatakiwa kujua kuwa si mazoezi yote huwa na faida katika upende wa kufanya mapenzi bali ni mazoezi ya Kigel ndio huwa na faida katika upande huu.

Kigel ni aina ya mazoezi rasmi yalioandaliwa kwaajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini kwa mwanaume na mwanamke.
Mazoezi haya husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawalisiliano, kuboresha udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia huimarisha uwezo wa kufanya tendo/mapenzi


Jinsi ya kufanya mazoezi ya kigel

Kitu kizuri kuhusu mazoezi haya ni hayahitaji gharama zaidi ya muda wako maana unaweza yafanya hata ukiwa nyumbani. Mazoezi haya hufanywa na wanaume au wanawake. Tafuta sehemu yenye hewa safi na nafasi ya kutosha pia iweinaruhusu wewe kulala chini (chini pawe pasafi au weka kitambaa), inaweza kuwa ni chumbani, sebleni na ikiwezekena nenda katika vyumba maalumu vya kufanyia mazoezi. Baada ya hapo unaweza fanya mazoezi yafuatayo;


Zoezi la kwanza;


Lala chali katika sakafu ilionyooka, kunja magoti kisha pandisha kiuno juu kabisa kama picha iliopo juu inavyoonesha. Baada ya kufanya hayo anza kupandisha kiuno hicho na kukishusha. Endelea kufanya hivyo kwa muda usiopungua dakika tano.



Zoezi la pili;




Jilaze katika sakafu ukiwa umenyooka na umeangalia chini, kisha unyanyue mwili wako kwa kutumia miguu yako na mikono yako kama jinsi picha inavyoonesha. Kaa kwa kuganda kama ulivyo na hakikisha wiliwako unanyooka kama rula kutoka miguuni hadi kichwani. Endelea kukaa kwa muda usiopungua dakika tano.



Zoezi la tatu;




Lala chali ukiwa umeinyoosha miguu alafu nyanyua mikono na miguu juu kisha kunja magoti miguu ikiwa bado ipo hewani. Anza kuushusha mguu wa upande mmoja wakati huohuo hukishusha mkono wa upende tofauti na uliopo mguu kisha rudisha tena mguu na mkono juu. Rudia kitendo hicho kwa mguu na mkono mwingine. Endelea kurudia rudia tena tendo hilo kama picha inavyooneshwa katika picha inavyooneshwa hapo juu kwa muda usiopungua dakika tano.





Hayo ni baadhi tu ya mazoezi ya kigel ambayo unaweza fanya kila siku ili kuuweka mwili wako uwe vizuri katika tendo la kujamiiana. Sasa tuangalie baadhi ya faida ambazo mtu anaefanya mazoezi haya huzipata.

Faida kwa mwanaume

  • Huongeza uwezo wa kujizui kumaliza tendo kwa haraka
  • Huimarisha misuli katika sehemu zake
  • Huongeza uwezo wa kubana mkojo


Faida kwa mwanamke

  • Huimarisha misuri ya nyonga na kuifanya iwe fanisi
  • Huongeza hamu ya kufanya mapenzi
  • Hufanya mzunguko wa damu ufanyike vizuri katika sehemu zake.


Natumaini mpaka umejifunza kitu nakusihi endelea kuwa na app ya Traah na hakikisha upo na sisi kila wakati ili uendele kupata vitu vizuri.







Previous Post Next Post