Jinsi ya kurudisha picha zote ulizowahi zifuta kwenye simu

 




Kurudisha picha zilizofutika ni Jambo ambalo watu wengi hawaamini lakini hili ni jambo la kawaida na linalowezekana pia. Kuna njia mbili ambazo unaweza zitumia kupata picha ulizozifuta. 

Njia ya kwanza ni kutafuta mafile yalio jificha na ya pili ni kutumia app zipatikanazo playstore. Njia ya kutafuta mafile yaliojificha huitaji uzoefu kidogo hivyo ni ngumu lakini hii ya App za playstore, ni rahisi na kila mtu anaweza ifanya.

Kuna app nyingi lilizopo playstore na zinauwezo wa kurudisha picha zilizofutika. Moja ya app hizo ni app iitwayo "Deleted Photo Recovery" Unaweza ipakua kwa kugusa INSTALL


Baada ya kuipakua fanya haya; 







  • Baada ya kuipakua, utaifungua na itakuletea ukurasa ambao unaeleza app inarudisha vipi picha. Utatakiwa kugusa neno "Restore" ili kuendelea, Kama jinsi picha inavyoonekana hapa chini.


  • Baada ya kufanya hivyo utaletewa ukurasa mwingine ambao ni wakuanzisha mchakato mzima wa kurudisha picha. Gusa neno "Restore Deleted Photo" ili kuanzisha mchakato huo Kama inavyooneswa katika picha.


  • Baada ya kufanya hayo, itaanza kutafuta picha zote na itakuletea idadi ya picha zilizopatikana. Gusa neno "Show Deleted Files" Kama inavyooneshwa katika picha iliopo chini ili kuziona izo picha zilizopatikana.




  • Baada ya kufanya hayo utaoneshwa mapicha mengi sana ambayo ni mchanganyiko wa picha zilizopo kwenye simu yako na picha ulizowahi futa. Utatakiwa kuzipiga tiki zile unazotaka kuzirudisha kisha utagusa sehemu ya chini yenye neno "Restore now". Ukigusa neno hilo, picha zitarudishwa na utaziona katika Orodha ya picha za kawaida.






.

App hii inauwezo wa kukurudishia zaidi ya picha 5000 ulizowahi zifuta kwenye simu yako. Ni rahisi kuitumia na watu wengi huitumia katika kuzirudisha picha zao.




Matokeo ya kuitumia app Ni mazuri 100% maana huzirudisha picha bila tatizo lolote ingawa Kuna baadhi ya simu huwa zinachelewa kuleta picha zilizorudishwa mpaka utakapo izima na kuiwasha simu yako.
Previous Post Next Post