Kuachana huumiza. Lakini kinachoumiza zaidi ni kujaribu kukumbuka ahadi zote mulizoahidiana ambazo sasa zimebaki zimetawanyika kama vipande vya nawe. Na mara nyingi unapokua umeumizwa huisi kuwa ni wewe tu ndio unapitia hali hiyo lakini ukweli ni kwamba karibu kila binadamu hukutana na hali hiyo baada ya kuachana na ampendae.
Kukabiliana na maumivu ya kuachana si rahisi. Lakini ili kukabiliana nayo inatakiwa uponya moyo uliovunjika, usahau ya zamani, na iwe rahisi kuyaepuka maumivu. Hapa kuna njia 14 za kukufanya utoke kwenye hali ya maumivu na kuwa mtu wa furaha kama zamani
1. Jipe muda wa kupona
Makosa makubwa ambayo watu hufanya baada ya kuachana ni kujishughulisha na shughuli za kujiharibu kama unywaji pombe kupita kiasi.
Jipe muda wa kupona. Anza kufanya mazoezi na kula kiafya. Pia, rudi kwenye burudani ambazo uliacha kwasababu ulikua kwenye mahusiano. Jaribu kujaza ratiba yako mambo ambayo yanakupa furaha na unayapenda kamwe usiwe na muda wakukaa bila kufanya kitu.
2. Usimfuatilie
Baada ya kuachana, labda unaweza kuwa unamfuatilia kwa siri katika mitandao ya kijamii ili ujue yupo wapi na anafanya nini.
Ili kuondokana na maumivu inakubidi uache kumfuatilia kabisa mtu ulieachananae maana kila unapoendelea kumfuatilia unazidi kuongeza maumivu katika moyo wako. Hivyo basi, block account zake za mitandao ya kijamii ili usiendelee kupata taalifa zake zozote zitakazo kuumiza.
3. Usitumie muda kumfikilia au kuangalia kumbukumbu za mahusiano yenu.
Huwa unaangalia picha zenu mulizokua mkipiga? Au unaangalia vitu alivyokua akikuzawadia?
Vitu mulivyokua mukivifanya au kuzawadiana inabidi viwe mbali na macho yako ili visikukumbushe na kukukosesha raha. Kama mulipiga picha ya pamoja na unajua hamuwezi hurudiana tena basi hiyo picha si kumbukumbu nzuri katika maisha yako hivyo basi iweke mbali kabisa na macho yako ikiwezekana ichome.
4. Kubaliana na ukweli halisi
Kama mmeachana na bado huamini kuwa mmeachana au hauamini kuwa unaempenda hawezi kuwa tena katika maisha yako basi utakua unaumia kila mara pindi unapona unaempenda hana ukaribu na wewe.
Kubaliana na hali halisi kuwa mmeachana na hamuwezi kuwa pamoja pia kuachananae si mwisho wa maisha yako.
5. Jifunze kitu kutokana na uhusiono wenu uliovunjika
Katika maisha kila mtu hujifunza kutokana na makosa. Ili usirudie kosa ni vema ukajifunza kitu juu ya mahusiano yenu yaliovunjika yaani kama ulimpenda mtu na ukampa asilimia zote za moyo wako na bado akaishia kukuumiza basi jifunze kutokumuamini mtu kiasi hicho kabla haujamchunguza vizuri.
6. Usitafute Visingizio vya Kukutana Nae Tena
Kuna wakati unatamani kujipitisha sehemu anayoshinda ili tu muonane? Au huwa unatafuta kila njia ili tu akuone ukidhani atakuita ili muyamalize?
Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kuwatokea ghafla mukaanza kupendana lakini pale yanapo yumba si rahisi kurekebishika. Hivyo usijisumbue kufanya akuone au muonane wewe endelea na maisha yako ya kuishi bila yeye maana kitendo cha kuonanane pia kinaweza changia kuongezeka kwa maumivu yako endapo atakuonesha ishara mbaya ya kutokukuhitaji.
7. Usiwe mtu wa kujilaumu.
Wengi huwa wanakumbana na tatizo la kujilaumu baada ya kuachana na wapenzi wao. Kamwe usitumie muda wako kujilaumu wewe au yeye yaani usiwe mtu wakujilaumu eti" kwanini nikimpa moyo wangu? Au kwanini hakuniambia mapema?" Hizi ni lawama zitakazo kufanya uanze kunywa pombe au kujiadhibu mwenye. Kitu cha msingi ni kupambana na hali ulionayo muda huu na kusonga mbele kila kujali chochote maana kunawatu wanakupenda zaidi hivyo kuondoka kwake ni furaha na nafasi nzuri kwa wanaokupenda kwa dhati.
8. Usijaribu kuwa rafiki yake wakati bado unahisia kwake.
Kamwe usijaribu kuwa rafiki wa mtu uliekuanae. Maumivu yako yataongezaka mara dufu. Ni vema kujitenga nae kabisa na kutoshirikiana nae kwa ukaribu ili tu kuunda moyo wako kwa kuyaona mambo yake. Unaweza kupewa kadi ya harusi yake na ukalazimika kufika kwasababu tayari mnaurafiki.
9. Jitambue na kujielewa
Kipindi ambacho mtu hayupo kwenye mahusiano ni kipindi ambacho mtu anaweza kufanya mambo yake binafsi na kupangilia mipango yake ikanyooka bila tatizo lolote. Hivyo basi, ni vema kutokaa kizembe tumia muda huo kufikilia wewe ni nani, unahitajika kufanya nini kisha anza kujishughulisha na mambo yako binafsi ili kujiweka sawa na pia kutimiza ulichokusudia kukifanya katika maisha.
10. Ondoa mawazo hasi kwenye kichwa chako.
Umekua ukifikilia kwa amekuacha kwasababu wewe ni mbaya au hunapesa? Kwanini ufikilie hivyo wakati wapo wengi wanaokupenda na kukuona wewe ni mzuri na pia wapo ambao wanatamani penzi lako tu na wala si pesa?
Acha kujikosoa na kuweka mambo mabaya katika kichwa chako. Weka fikila za kwamba yeye ndio amekukosea tena hutaki hata kumuona kisha ziweke kichwani faida za kuachananae. Sawa mmeachana lakini so alikua anakuomba hela kila Siku? Sasa huoni kuondoka kwake ni faida? Au uliwahi mfumania Mara nyingi Sasa huoni kuwa angekuoa ungeteseka zaidi?
11. Jinunulie vitu unavyovipenda
Usichokijua ni kwamba, kununua vitu unavyovipenda kunaweza irudisha furaha yako kwa kiasi kikubwa. Nunua nguo nzuri zinazokufanya uwe na muonekano mzuri na mpya au tumia hela zako katika manunuzi ya vitu vingine vinavyo kufurahisha kama vile games, vyakula vitamu na juice.
12. Tumia muda na marafiki zako.
Marafiki ni watu wanaweza kukufanya ukasahau shida na maumivu yote ulionayo. Pindi unapokua na muda basi fanya kujichanganya na marafiki ili mufurahi kwa pamoja. Hii itaweza kukufanya ufurahi na uchukulie kuachwa au kuachana ni jambo la kawaida hasa pale unapowasimulia.
13. Usiingie kwenye mahusiano mpaka upone kabisa.
Kama moyo wako bado una maumivu usijaribu kuingia kwenye mahusiano. Watu wengi wameyachukia mapenzi kwa kutozingatia hili, yaani anaumizwa na mtu alafu anaingia kwenye mahusiano mengine akifikili atapona maumivu yake lakini badala yake anaumizwa tena na huyo huyo aliefikili atamtuliza. Ni vema kujipa muda wa kutosha kabla haujaingia kwenye mahusiano mengine.
14. Jipende mwenye
Wewe ni mtu pekee unaetakiwa kujipenda na kujisifu kabla ya mtu mwingine. Hakuna mtu anaeweza kukuumiza kwa kukwambia hakupendi ikiwa wewe mwenyewe unajipenda. Tambua thamani yako maana kunawatu wanakuona wathamani japo hawakwambii. Jiamini kwakua wapo watu wanao kuamini japo hawaja kwambia.
Tambua kwa mulieachananae ni kipofu asieona thamani yako,wewe ni wathamani kuliko anavyofikili.