Utajuaje simu yako imeunganishwa na mtu anaekuchunguza?

 


Mtu kupata SMS na Calls za mtu mwingine, limekua ni jamabo rahisi sana katika ulimwengu wa sasa kutokana na kuwepo kwa njia nyingi za kufanikisha jambo hili. Lakini kuna faida dogo na hasara kubwa za kumfanyia mtu Jambo hili hasa katika mahusiano amboko ndio Jambo hili hutendeka zaidi. Watu wengi wamejikuta wamefanya mambo ya ajabu kwa wapendwa wao kutokana na kuweka vitu hivi na cha kushangaza, mtu anaemuwekea mwenzake huwa hapendi kuwekewa kutokana na kutojiamini... Sasa kwanini umuunge mtu bila kumtaarifu wakati wewe hupendi kufanyiwa hivyo? 

Katika post hii nakueleza jinsi gani unaweza tambua simu yako imeungwa na mtu mwingine ili apate SMS na Calls zako bila wewe kujua. Lakini utafanikisha hili kama mtu huyo ametumia huduma ya Call Forwarding kukuchunguza.
 
Jinsi ya kutambua
Fungua sehemu ya kupiga simu na uandike namba *#62#  kisha piga.

Baada ya kupiga, kama utaletewa orodha ya maneno yalio na neno "Not forwarding" basi tambua ujaungwa na huduma hii.



kama umepata matokeo mbali na hayo basi unaweza kuwa umeungwa na huduma hiyo na unachotakiwa ni kupiga ##002#  ili futa huduma hiyo kabisa.


Kitu cha muhimu kukijua ni kwamba, kumchunguza mtu bila ridhaa yake ni kosa kisheria!.



Previous Post Next Post