Jinsi ya kumueleza hisia zako Mwanaume bila kusema unampenda

 




Mara nyingi kuwa na aibu ndio chanzo cha wanawake wengi kushindwa kuwaeleza hisia zao kwa wanaume wanao wahitaji na kibaya zaidi wanawake tunaweza kutunza siri zetu kwa muda mrefu hivyo, hutunza pia hizo hisia kama siri nyingine japo hutuumiza sana pale wanaume tunaowapenda  wanapoenda kwa wanawake wengine.

Wapo baadhi ya wanawake ambao hawana uoga katika kueleza hisia zao kwa wanaume na pia huwa huru pindi wanapokuwa karibu na wanaume. Lakini wanawake wengi ni sisi ambao tunashindwa hata kuongea pindi tunapo wakaribia wanaume tunaowapenda.

Sio kwamba tunakosa ustadi wa kimapenzi wa kimapenzi au hatujui kutamka maneno ya kueleza hisia zetu ila ni tunasikia raha na furaha inayotuzidi mpaka tunaogopa maana mapigo ya moyo hupiga kwa kasi na maneno yote hupotea na hurejea baada ya mwanaume uondoka.

Kuwa na aibu hakupaswi kukuzuia kumueleza mwanaume unayempenda hisia zako. Kuna mambo madogo madogo ambayo unaweza kuyafanya na ukafanikiwa kufikisha ujumbe wa hisia zako kwa mwanaume unayempenda lakini kitu cha msingi inatakiwa kujiamini tu.

Badala ya kumfuata na kumwambia mwanaume vile unajiskia juu yake unaweza tumia njia ya vitendo itakayo mfanya kukuzingatia na kuelewa kuwa unamuhitaji na utamfanya akuhitaji pia.

1. Wasiliana nae kwa macho.



Kuwasiliana kwa macho ni moja wapo ya njia rahisi na ya hila zaidi ya kumruhusu mwanaume ajue kuwa unavutiwa naye. Wakati mwingine wazo la kuwasiliana na mtu usiempenda linaonekana kuwa la kichefuchefu, lakini ikiwa unafikiria ni mzuri, muangalie. Kama ni muoga sana basi jaribu kuangaliana na picha yake kwenye simu yako. Usimtazame kama wewe ni polisi na yuko kwenye orodha ya watu wanaotafutwa. Mtazamo mfupi ndio unahitajika yaani muangalia mpaka ugonganenae macho na agundue ulikua unamungalia kisha acha kumuangalia na uiangalie sehemu nyingine (ila usingalie chini kamwe) huku ukiendelea na shughuli zako. Kitendo hiki ukiwa unakifanya kitamfanya ahisi kitu juu yako na anaweza kuanza mawazo ya upendo juu yako.

2. Weka tabasamu.




Pindi unapomuangalia hakikisha anakukuta na tabasamu zuri la kupendeza. Sio anakukuta unamuangalia huku umeweka sura ya kawaida tu utamfanya asihisi chochote juu yako na akakuona ni mtu unaemfuatilia mambo yake hivyo hakikisha unaweka tabasamu zuri litalomuonesha kufurahishwa na yeye. Akikukuta katika hali hii moja kwa moja atagundua umevutiwa nae.


3. Muulize swali kuhusu jambo flani.





Hii ni njia nzuri sana kwaaji ya kuanzisha mahusiano kati yenu.
Kuuliza swali kuhusu jambo flani au kuomba usaidizi juu ya jambo flani. Unaweza muuliza mwaswali ambayo yatamfanta ajibu kwa urefu au atumie muda wake kukuelekeza.

Mfano: Eliy, nimependa wallpaper ya simu yako, naomba nielekeze jinsi ya kuweka wallpaper kama yako?

Naomba nielekeze jinsi ya Download status za WhatsApp?

Njia hii pia utakusaidia kuanzisha mazungumzo nae yaani pale unapokosa neno la kuongea au kuanza mazungumzo basi unaweza uuliza kuhusu kitu flani.



4. Mtege kwa kujichezesha.



Kila mwanamke anavitu ambavyo anajua vinamshawishi zaidi mwanaume katika mwili wake. Vitu hivi vinaweza kuwa ni lips nzuri, macho na vinginevyo. Vitu hivi unaweza vitumia pale ambapo unakuambele ya macho yake au unapogundua anakuangalia. Kuvitumia vitu hivi kunaweza kumchanganya mwanaume kisawa sawa mpaka akashindwa kuongea na kumfanya avutiwe na wewe zaidi.

 Mfano, unaweza zichezesha lips zako pindi anapokuangalia na kukuelekeza kitu fulani ulicho omba akuelekeze.

Kwakufanya vitendo Kama hivi kutachochea hisia zake kwako.


5. Toa maoni juu ya kile unachokiona kwake na pia usisahau kumsifia na kusifu anavyovipenda.



Kila mtu anapenda kusifiwa na  sikuzote watu huwapenda watu wanaowasifu pia unachotakiwa kujua ni kwamba  wanaume wengi huongeza juhudi katika jambo fulani pale wanaposifiwa yaani kama ni mchezaji mpira alafu ukawa unamwabia kuhusu uchezaji wake mzuri wa mpira basi utamfanya ajiskie vizuri mpaka ataanza kukualika mazoezini ili tu umuone anachokifanya na umsifie tena. Hivyo basi kumsifu inaweza kuwa njia nzuri ya kufanya avutiwe na wewe.




6. Usichukue vitu kibinafsi.




Ikiwa umemfanyia yote hayo na bado haoneshi matokeo mazuri juu yako, Usihisi kuwa wewe ni mbaya au hunamvuto. Huenda haoneshi dalili nzuri juu yako kwasababu hataki kukuchezea hivyo unapaswa kuheshimu pia mawazo yake na kuendelea na maisha yako huku ukimtafauta anaekupenda kwa dhati. 



Previous Post Next Post