Sms za kuomba msamaha kwa mpenzi wako

 



Mpenzi wangu naomba unisamehe, nakupenda sana dear na ni kweli kuna wakati nakukosea, lakini amini nakupenda sana na sijawahi kujuta wala sitajuta kamwe kuwa na wewe! Naamini nitaendelea kuwa mwaminifu kwako, sio leo tu, bali siku zote za penzi letu hapa duniani!



Tukae kimya sheteni apite, kamwe tusimruhusu afanikiwe kuvuruga uhusiano wetu. Naamini haikuwa akili yangu bali ni ushawishi wa sheteni ambaye siku zote amekazania kuharibu penzi letu! Nisamehe wangu.




Wewe ni taa kwangu imulikayo gizani, nakupenda sana mpenzi wangu wa moyo, utakuwa wangu siku dear! Kosa nililofanya ni kwa bahati mbaya mpenzi wangu, naomba unisamehe na ninaahidi kutorudia tena katika penzi letu!



Tega sikio dear, nakupenda sana, ukweli wa ile sms uliyoifuma kwenye simu yangu, haikuwa yangu bali mtumaji alikosea kwa bahati mbaya! Nipo tayari tumpigie tukiwa pamoja tumuulize, kweli niamini dear! Naomba usiniache maana maisha yangu bila wewe ni sawa na giza nene!



Mimi kwako ni kipofu, nishike mkono tuvuke barabara, magari ni mengi na yanapita kwa kasi, siwezi kuona zaidi ya kusikia yakiunguruma, honi za magari siwezi kupima umbali wake, usiniache katikati ya barabara nitagongwa na kufa mara moja! Njoo niokoe nitagongwa mpenzi wangu! Forgive me dear…



Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!



maneno million haliwez kulirudisha pendo lako najua kwasababu nimejaribu,pia machozi million haliwez kulirudisha najua kwasababu nimelia. Lakini tambua halikua kusudi langu, unaniumiza bure.



Najua nimekukosea mpenzi, lakini fahamu kwamba
haikuwa nia yangu kukupotezea furaha yako, kwakua wewe ndie mtu pekee ulieushika moyo wangu. Tafadhari nipe
nafasi nyingine moyoni mwako!
Nipe nafasi nyingine maishani mwako!
Nisamehe mpenzi wangu!







Previous Post Next Post