Jinsi ya kujua kama akaunti ya Facebook imeingiliwa na mtu/inachunguzwa

 





Kama unataka kujua account yako ya Facebook hua inaingiliwa na mtu mwingine kisiri,kuna mtu anaijua password yako na unamtilia wasiwasi au uliwahi login kwenye simu ya mtu bila Ku logout basi fuata Yafuatayo;

1. Ingia katika Facebook yako alafu gusa "Menu" yaani vimistari vitatu vya ulalo upande wa kulia juu.

2. Ukisha gusa Menu itakuletea orodha ya vitu vingi sana wewe tafuta neno "settings" kisha ingia Kwakuigusa.

3. Kwenye settings pia kuna vitu vingi, tafuta neno "Security and Login" kisha ingia Kwakugusa.

4. Ukisha ingia utakuta orodha pia lakini tafuta "WHERE YOU'RE LOGGED IN" kisha ingia hapo utapata orodha ya simu au PC zilizotumika kuingia katika Account yako,muda,mahali simu hizo au PC zilipo, zimetumia browser ipi na kifaa unachotumia kwasasa.

Kama utakuta simu ambayo hutumii katika orodha au sehemu tofauti na ulipo na kwa muda ambao hukutumia Facebook jua kunamtu tofauti aliingia.

Kama kuna simu au PC ulilogin ukasahau kulogout bc unaweza kulogout hapo hapo kwenye list.



Previous Post Next Post