Kwanini wanawake warembo hawaolewi?




Mara nyingi wanawake warembo na wenye mvuto wa kumvutia kila mwanaume huishia kuzisikia ndoa kwa wenzao tu kutokana na sababu mbalimbali.
Wengi huwa na tabia ambazo huudhi na huwaogopesha wanaume wanaowahitaji bila wao wenyewe kujijua.

Ivi unaweza kuchagua kuwa na kitu chenye muonekano mzuri maishani mwako kitakachokupa shida na maumivu milele?
Ikiwa watu hushindwa kuvumilia kuishi na vidonda vinavyowapatia nyumba, magari na pesa, unafikiri urembo/uzuri unaweza kuwa na nini cha ajabu kwenye maisha?

Wanaume huwa sio wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni wanawake wa kawaida sana ukiwaangalia kwa macho jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza "mbona kamchagua mwanamke wa kawaida sana pamoja na malizote zile?"

Ukiwa mrembo/mzuri utapendwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo la kupata Penzi tu, baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na baadhi ya sababu zinazopelekea wanaume kufanya hivyo ni zifuatazo;


 

Tabia



Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na nikiongelea tabia mbaya basi najumuisha uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri na marafiki pia. Vitu hivyo humtenganisha mwanamke mzuri na wanaume wa oaji. Labla akutane na mtu wa tabia yake lakini asilimia kubwa ya wanaume wenye tabia hizo huwa wanatafuta wanawake waliotulia huku wakiendelea wanawake warembo wasio tulia. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awemrembo kiasi gani.

 

Kuwa na maringo sana



Unakuta mwanamke ameweka kucha ndefu, nzuri,za kuvutia na anamaringo kiasi kwamba mwanaume mwenye mpango wa kuoa akimuona anajiuliza 
"Sasa kwa hizi kucha atanifuliaje nguo?... Anamaringo sana sijui itakuaje tukipishana?... Anaanzaje kuosha vyombo?... Ivi atakubali kutulia na kulea mtoto?.. Inaonekana hata kupika hajui"

Mwisho mwanaume anaona hafai wala haoneshi tabia zozote za mwanamke ambae anatakiwa kukaa katika nyumba.


 

Ghali kuwatunza



Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu wamejiwekea dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.
Mwanaume akipiga hesabu za haraka haraka kuhusu ghalama ambazo anatumia kipindi cha ambacho yupo na mwanamke mrembo anaependa kulidhishwa kwa kufanyiwa mambo makubwa huwa anagundua kumuoa ni sawa na kubeba mzigo mzito sana kichwani.


 

Ni wabinafsi



Wanawake wa aina hiyo huishi wakifikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuwa katika mahusiano nao na hii ndio sababu kubwa ya wanawake hawa kujiona wa hali ya juu sana.

Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa. Kibaya zaidi ni kwamba, wanawake hawa huendelea kutiwa moyo na uzuri wao huku wakisahau kuwa umri walionao hauwasubiri.

 

Hawataki kuwa wazazi



Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wanapendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika. 

 

Sasa kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume. 







Previous Post Next Post