Sikukusudia: 01 (Simulizi)




SEHEMU : 01

Asubuhi na mapema, kijana Jimmy aliamshwa na muito wa simu yake iliokua ikimuita muda huo. Alichukua simu na kuipokea. 

"Eee hallo!" Jimmiy alisema huku akiwa hamjui hata aliekua akimpigia kutokana na namba kutokua na jina.

Alisikia sauti nzuri ya mrembo Suzi ikisema "Sorry Jimmy kwa kukusubua asubuhi hii, Mimi ni yule dada ulienipaka rangi hapa katika duka la vitenge alafu nikaomba namba yako"

"Anha nimeshakupata.. ni vipi Suzi?" Jimmy aliongea huku kifuraha kikimjia kwa mbalii baada ya kugundua kuwa anaongea na mrembo suzi.

"Safi tu... Nilikua nahitaji unipake rangi kwenye kucha za miguu leo alafu kunakitu nahitaji tuongee pia Jimmy" Suzi alimwambia Jimmy.

"Sawa Kwaiyo nije sasaivi?" Jimmy alimuuliza Suzi.

"Hapana, nimekupigia nikutaalifu tu maana hata dukani leo sitakuepo" alisema Suzi.

"Duh! Kwaiyo itakuaje sasa!?" Jimmy alimuuliza Suzi

"Mimi leo niko nyumbani tu. Kwakuahupajui nyumbani kwangu, ikifika saa8 mchana nenda katika duka langu tulipokutana utamkuta mfanyakazi wangu tu,nipigie ukiwa hapo alafu nitatuma bodaboda wa kuleta hadi kwangu" Suzi alimwambia Jimmy

Jimmy alimuelewa Suzi" Sawa nitafanya ivyo"

Baada ya mazungumzo hayo walitoa simu masikioni na Jimmy alikua na furaha sana kwani alitokea kumpenda sana Suzi pia alihisi kitu anachoitiwa na Suzi ni mapenzi tu na si rangi maana Suzi alionesha dalili za kuvutiwa na Jimmy tangu walipo onana. Suzi ni mke wa mfanya biashara mkubwa sana lakini Jimmy hatambui chochote zaidi ya kuhisi kuwa Suzi ni dada kwenye pesa zake.

Jimmy alijisemea "leo asipo niambia lazima nitamwambia... Toto limeshainielewa na siweziacha bahati hii" 

ENDELEA KUSOMA SEHEMU YA PILI KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH...


Previous Post Next Post