MKASA WA KWELII’’’’
NA CLEMENT CHARLES
……………Ilikuwa ni siku iliyoonekana ya kheri toka asubuhi yake kwani mamdogo alikuwa akipanga vitu vyake kwa ajili ya safari ya kwenda kumsalimia shangazi yake huku tumboni akiwa amebeba kiumbe ambacho muda wa kuletwa kwake duniani ulikuwa umekaribia. Tulimuaga mamdogo kisha tukamsindikiza mpaka stendi ya mabasi ambako alichukua moja kwa moja basi lililokuwa likielekea kijijini kwa bibi (kwa shangazi yake) baada ya hapo tulimsindikiza kwa macho mpaka lile basi aina ya yutong lilipopotea katika mboni ya macho yetu kisha nasi tuliishika njia kurudi nyumbani huku moyoni mwetu tukiwa tunatia nia mamdogo afike salama huko aendako na mola amsimamiee.
Mungu si Athumani majira ya jioni mamdogo alipiga simu majira ya jioni na kututaarifu kuwa safari aliyokuwa ameiendea amefika salama salimini tena bila tatzo lolote, sisi kama ndugu zake na watoto wake tulishusha pumzi na kumshukuru mola kwa kumfikisha salama kwani safari ni jambo gumu pia kwani safari nyingi huwa hazitabiriki na huwa zinakuwa na misukosuko ya hapa na pale ‘’Allhamdulillahi mwenyezi mungu umemfikisha mamdogo salama kwani kwa hali aliyokuwa nayo anahitaji uangalizi wa hali ya juu’’ nilijisemea maneno yale kimoyomoyo.
BAADA YA SIKU TATU KUISHA
Tulipigiwa simu na bibi (shangazi yake mamdogo) akituelezea kuwa hali ya mamdogo imebadilika na wamemkimbiza hospitali mara moja kwa ajili ya matibabu na wataalamu wameshauri alazwe kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi. Mama yake mamdogo (ambae kwangu ni bibi) alilipokea jambo hili kwa mashaka sana na ilipofika asubuhi ya kesho yake alijiandaa haraka haraka na nilipomuuliza ‘’bibi unaenda wapi’’ ‘’naenda kwa mamdogo wako nimepigiwa simu amezidiwa’’ .
Daaah lile jambo lilizidi kukiumiza kichwa changu na ndipo masikio yangu nikayaelekeza kwa wakubwa kusubiria kilichotokea huko kwani bibi(mama yake mamdogo) kwani angetuletea majibu ya yale yaliyotokea huko aliko mamdogo.
BAADA YA SIKU MOJA KUISHA
Tuliitwa asubuhi na kuambiwa tujipange kumpokea mamdogo kwani alijifungua mtoto , kisha mtoto yule alifariki INNALILLAHI WAINNAILLAIHI RAJIUN jambo lile liliuuhuzunisha sana moyo wangu. Baada ya muda waliwasili na tukapewa kazi ya kuaanda mahali pa kumsitiri mdogo wetu yule aliyetoka katika tumbo la mamdogo. Tulimaliza kazi ile kisha tukaanza zoezi la kumuosha mdogo wetu mpendwa ambae nae alikuwa kidume (wa kiume) kisha tulipomaliza kumuosha kwa uangalifu mkubwa tulimkafini kwa ajili ya kwenda kumstiri.
Baada ya hapo tuliwaruhusu wanawake kwenda kuuchukua kuuchukua mwili na kuupeleka mahali pa kuzikia nami nilitangulia kaburini kuupokea mwili wa mdogo wangu mpendwa tayari kwa kumpumzisha katika mwana ndani baada ya hapo nilifanya yote kisha nikiiongoza dua ya kumwombea mdogo wangu yule ambae hata safari ya dunia alikuwa hajaianza. Kiukweli niliisoma dua huku mikono ikinitetemeka kwani sikuwa kuamini kile kilichotokea na mwili uliniisha nguvu basi nilijitahidi kuomba dua baada ya walifukia kisha tukaenda kukaa kupumzika kusuburi taratibu zingine.
Ila jambo linaloniumiza kichwa na kuzidi kunipa machungu moyoni ni hili HIVI INAKUAJE MWANAMKE ANABEBA MIMBA MIEZI TISA AFU SIKU ANAJIFUNGUA SALAMA NA MTOTO ANAFARIKI SIPATI PICHA NI MACHUNGU KIASI GANI ANAYAPATA MOYONI MAMA WA YULE MTOTO kila nikikaa na kulikumbuka hili jambo mwili unaishiwa nguvu kabisa na kuzidi kumkumbuka mdogo wangu ambae hatunae tena ila namwombea kwa mola ampumzishe salama amiin..
CLEMENTI - "NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA MWENYEZI MUNGU NA MAMA YANGU ALIENILEA MPAKA NIMEFIKA HAPA KWANI SIJUI NI MACHUNGU KIASI GANI AMEPITIA MPAKA NIMEFIKA HAPA. NAPIA NIWAPE POLE WAKINA MAMA WOTE WALIOWAPOTEZA WATOTO WAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE"