Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye friji (Jokofu)



Sababu kubwa ya friji kuwa na harufu mbaya huwa ni bakteria ambao hutokana na vitu tunavyoweka kilasiku katika friji (Majokofu) zetu.

Endapo itatokea friji lako limeanza kutoa harufu mbaya Basi unaweza fanya nyafuatayo ili kuiondoa kabisa harufu hiyo mbaya katika friji kwa urahisi.


1. Ondoa kila kitu katika friji



Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha friji haina kitu ndani yake. Ondoa vitu vyote ambavyo umeweka katika friji hiyo na uliache friji likiwa halinakitu ndani yake.

2. Safisha friji 



Baada ya kuondoa kila kilichokua katika friji, chukua maji na uanze kulisafisha ili kuondoa uchafu au mabaki ya vitu vilivyokua katika friji. Hakikisha unasafisha kila sehemu ya friji kwa kutumia maji safi maana vitu vingi vinavyowekwa katika friji ni vitu ambayo vinaenda vinywani mwetu.



3. Futa friji kwa maji yenye soda.


Hapa tunazungumzia baking soda. Baking soda ni unga ambao mara nyingi hutumika katika utengenezaji wa maandazi. Kama utakua bado huufahamu basi nenda kwa mpika maandazi yoyote yule anaeishi karibu yako na umuulize kuhusu hii.

Sasa unachotakiwa ni kuanda maji lita mbili(2) kisha weka unga wa baking soda, vijiko vitatu au vinne  kisha changanya kisawa sawa.
Baada ya kuchanganya, chukua kitamba safi na utumie kusafisha tena na kulifuta friji hilo kwa mchanganyiko huo. Mchanganyiko huu ndio huondoa harufu katika friji.

4. Rudishia vitu kwa mpangilio.


Baada ya kulifuta anza kurudishia vitu kwa mpangilio maalumu na Kama unavitu vinavyotoa harufu kama vile nyama na baadhi ya matunda basi hakikisha unaviweka katika vifungashio maalum ili kuzuia harufu mbaya kwa wakati mwingine. 

Kitu cha msingi unachotakiwa kukijua ni kwamba harufu haitakata muda huohuo unaosafisha bali itaanza kukata wakati umemaliza kila kitu maana inawezakuchukua hata zaidi ya saa1 lakini mara nyingi haizidi masaa mawili(2)

 


Previous Post Next Post