Mfahamu msanii aliepachika jiwe la Almasi katika kichwa chake



Tumekua kutiona baadhi ya wasinii wakifanya vitu vingi sana vya ajabu kwa nia ya kujiremba au kujiweka tofauti lakini hii tunaweza sema ni kitu kikubwa na cha ajabu kilichofanywa na msanii wa kimalekani ajulikane kama Lil Uzi Vert.

Lil Uzi Vert amezua hisia kali mtandaoni baada ya kutumia takribani $24m ambazo ni sawa na Tsh 55,716,000,000 kwa Tanzania , kununua almasi yenye karati 11 na kuipandikiza katika paji lake la uso , hatua iliowashangaza watu wengi sana Duniani.

Baada ya kupandikiza Almasi hiyo katika paji la uso akatuma video fupi katika akaunti yake ya Instagram. Video hii unaweza iangalia hapa.



Lil Uzi Vert ni (Symere Bysil Woods) ni mwanamuziki wa Marekani wa muziki aina ya Rap ambae ni mtunzi pia.


Alizaliwa mwaka 1994, Kaskazini mwa Philadelphia huko Francisville, nchini Marekani.

Mwanamziki huyu alianza kufahamika zaidi katika mwaka 2015 baada ya kutoa wimbo wake wa Lov is Rage.








Previous Post Next Post