Unasumbuliwa na kelele za SMS za magroup ya WhatsApp?

 



Wengi tumekua tukitumia WhatsApp katika kuwasiliana na ndugu na jamaa zetu kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pia tumekua tukijiunga katika Magroup (Vikundi) ambavyo nia na madhumini yake ni kutujumuisha kwa pamoja ili tuweze kujadili au kubadilishana mambo mbalimbali. 

Kuwa na group si tatizo ila tatizo huja pale group linapokuwa na watu wengi wanaochati kipindi wewe hauna muda wa kuchati kutokana na sababu mbalimbali na kukupelekea kuona sms za wengine kuwa kero kwakua huingia kwa kelele mfululizo.

Kama unagroup ambalo husababisha kelele kutokana na message zake, unaweza lifanya yafuatayo ili kulifanya liingize message kimya kimya;

  • Nenda katika ukarasa wako wa WhatsApp kisha lishikilie group lenye kelele kwa muda usiopungua sekunde tatu Kama inavyooneshwa hapo chini.


  • Ukishikilia kwa muda wa sekunde tatu group litajipiga tiki na maeneo ya juu ya WhatsApp kutatokea chaguzi: katika chaguzi hizo utaona alama ya spika iliokatwa. Alama hii inamaanisha kulikarisha kimya group hivyo utaigusa alama hiyo kama picha inavyokuonesha hapa chini. 


  • Baada ya kuigusa alama hiyo utaletewa chaguzi uchague group hilo liwekimya kwa muda gani kwaiyo utachagua masaa8, wiki 1 au milele kisha utagusa neno "Ok" kama inavyooneshwa katika picha.



Baada ya kufanya hayo utakua umetatua tatizo la kelele maana sms za group hilo zitakua zinaingia kimya kimya. Na unachotakiwa kujua ni kwamba kama utachagua masaa8 basi baada ya masaa8 group litakua linaingiza sms kwa kelele kama kawaida na hata ukichagua wiki, wiki likiisha kelele zitakua palepale ila ukichagua milele hutaskia kelele za group hilo mpaka utakapo lishikilia tena group hilo na kugusa kialama cha sipika isiokatwa ili kuliweka huru.

Kama ni mtu ambae unamagroup mengi au unamagroup ya ajabu ajabu unaweza tumia njia hii kuepuka kelele na kulifanya group lisijekukuumbua na taalifa za sms za ajabu ajabu.


Previous Post Next Post