"We na wee... huishi kunisifu. Tusije tukakesha hapa, ngoja nikafanye kazi zangu"aliongea Rose huku akibeba maji na kuondoka kisimani.
Jimmy alibaki akicheka huku akimsindikiza kwa macho binti Rose akiwa anatembea huku akitikisa mizigo yake ya nyuma mithiri ya maji ya viroba ili kuichanganya vilivyo akili ya Jimmy ambae wanamahusianonae ya kimapenzi kwa muda wa miaka miwili sasa na Rose anampenda sana Jimmy kiasi kwamba alikataa kuendelea na shule yaani kwenda form V kwa visingizio vingi sana kwa mama yake lakini ukweli ni kwasababu aliahidiwa kuolewa na Jimmy lakini kutokana na maisha ya Jimmy kuwa magumu... siku zinakwenda tu na hakuna kinachoendelea zaidi ya kutoroka kwao usiku, kutumiwa na Jimmy usiku kucha kisha kurejea alfajiri... Muda mwingine mchezo huu unamfanya Jimmy amchoke Rose na ndiomaana hapokeagi simu zake za usiku na kibaya zaidi ni kwamba moyo wa Jimmy unaanza kutekwa na Suzi kipindi ambacho Rose anataka kumwambia Jimmy kuwa anadalili za ujauzito.
Basi akili ya Jimmy ilihama kwa sekunde chache kutokana na ile mitetemo lakini akili iliporejea akakumbuka kitu kikubwa ambacho anatakiwa kukifanya siku hiyo...
Alichukua maji haraka na kuelekea bafuni kuoga kisha akarudi katika chumba chake. Aliziangalia mara mbilimbili nguo alizoandaa kwaajili ya kwa mrembo Suzi huku akijipa moyo kwa kujisemesha "Hapa ndege haruki... Hapa... Natua kama mnyamwezi... Hahah.. atarukia wapi?!" Kisha akavaa nguo nyingine ambazo ni maalumu kwaajili ya kazi alafu akatupia begi la vifaa mgongoni na kushika kikapu maalumu kilichojaa chupa za rangi za kucha.
Baada ya kujiweka tayari, alitokanje na kuufunga Mlango wa chumba chake kimoja alichukua akiishi kwa kufuri moja zito Sana ili kuvilinda vituvyake maana mtaa aliokuaanaishi ulikua ni wakiswazi na wenye wezi wengi sana.
Baada ya hapo alivutapumzi na kuianza safari ya mtaa kwa mtaa ili kuwapaka rangi na kuwasafisha kucha watu wanao hitaji huduma hiyo...
Alipita mtaa kwa mtaa huku akili yake ikiwaza juu ya Suzi tu na kumpelekea kila muda aweanaangalia muda kwenye saa katika simu yake. Siku hiyo ilikua mbaya kwake kwani hakupata hela nyingi kutokana na akili yake kutokujikita katika kutafuta wateja.
Mpaka kufikia saa6 alikua amefika mbali Sana na alipata hela ya kula tu. Jimmy aliamua kuanza safari ya kurejea nyumbani na wakati akikaribia kwake aliaona si vibaya Kama ataingia katika magahawa ambao ulikua mtaa watatu toka kwake kwaajili ya kupata chakula.
"Ahaa Jimmy... Ndio ninachokupendeaga Shem langu huchoki kuniungisha" Ilikua ni sauti ya Sophia akimkaribisha Jimmy pindi alikokua anaingia
UNAFIKILI NI KWANINI "SHEM"?
JIMMY ATAZICHUKULIAJE TAALIFA ZA UJAUZITO WA ROSE IKIWA KWA SASA HAYUPO MOYONI?
ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU INAYOFUATA KUPITIA APP YAKO BOMBA YA TRAAH