Nge ni mmoja wa wanyama wenye sumu kali sana na sumu yake inaweza sababisha mtu kupooza mwili au kupoteza maisha japo baadhi ya aina za Nge huwa hawana sumu zenye athari kubwa.
Kuna zaidi ya aina 1800 za Nge ulimwenguni na kila Nge hutoa sumu tofauti. Nge huwa na miguu nane, macho 6 hadi 12 na mkia mrefu wenye mwiba ambao huutumia kudunga windo na kuiingiza sumu ndani yake.
Nge wadogo huwa wadudu wadogo wadogo lakini kuna Nge wakubwa ambao hula mijusi na panya.
Mbali na sumu ya Nge kuwa ni hatari lakini imekuwa na umuhimu mkubwa katika maswala ya afya ya binadamu. Wanasayansi hutumia sumu hii kutengeneza madawa ya kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali hasa matatizo ya ubongo na kupambana na kansa.
Kwa sasa sumu ya Nge ni moja ya vimiminika vinavyouzwa bei ghali ulimwenguni ambapo inakadiliwa kwa Gramu moja tu ya sumu ya Nge inaweza kuwa zaidi ya Tsh 16,000,000.
Lakini sababu kubwa ya sumu hii kuwa ghali sio umuhumu wake bali ni mchakato ambao unatakiwa kufanyika ili kuiandaa na uzalishwaji wake ni mgumu kwakua Nge huzalisha kiasi kidogo mno cha sumu kila baada ya wiki mbili.